Sunday, April 30, 2017

MBUNGE WA BUKOMBE AWATAKA WANANCHI KUVUNJA MAKUNDI YA VYAMA NA KUWA WAMOJA

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dotto Biteko akiwa kwenye Mkutano wa kutatua na kusikiliza Kero za wananchi kijiji cha Bwenda Kata ya Kantente.
Meza Kuuu hakiwepo Mbunge wa Jimbo la Bukombe pamoja na viongozi wa Kijiji cha Bwenda na wa kata ya Kantente. 
Wananchi wakitoa kero zao mbele ya Mbunge wa Bukombe. 
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dotto Biteko akikabidhi mpira kwa Mwenyekiti wa Kijiji ambayo ilikuwa imeombwa na vijana kwaajili ya kujiandaa na Kombe la Dotto Cup 
Diwani wa Kata ya Bulangwa Yusuf Mohamedi akielezea wananchi juu ya serikali ambavyo imejipanga kutatua Kero za wananchi juu ya Elimu pamoja na Huduma ya Afya.


Wananchi wa jimbo la Bukombe Mkoani Geita,wametakiwa kuachana na siasa ambazo zinaweza kusababisha kutokuwa wamoja katika kuleta maendeleo.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Jimbo la hilo Dotto Biteko wakati akizungumza na wananakijiji wa kijiji cha Bwenda Namba 9 Kata Ya Kantente ambao ulikuwa na lengo la kusikiliza Kero za wananchi na kutatua changamoto walizo nazo.

Amesema kuwa maendeleo ya sehemu yoyote hile hayawezi kuletwa kwa watu kutokuwa na umoja na upendo.

"Wana Bwenda inahitajika nguvu ya pamoja ili kuhakikisha tuna maliza changamoto za eneo letu, zikiwemo ukosefu wa miundo mbinu ya barabara, kituo cha Afya, miradi ya maji na kuzorota kwa ufaulu wa wanafunzi na niombe wazazi mshirikiane na walimu kwa kufuatilia kwa ukaribu zaidi maendeleo ya vijana mashuleni" Alisisitiza Dotto .

Hata hivyo ameongezea kuwa kwa vijana wameanza kutenga asilimia kumi ya mapato na tayari vikundi kumi vimekwisha kupatiwa Mkopo na kwamba ameshapata fedha nyingine ambazo ni milioni hamsini na moja kwaajili ya maendeleo na mikopo kwa vijana na wanawake.

Pia amewataka wanakijiji hao kutokuwaogopa viongozi wao na kuwaambia kama wameshindwa kutekeleza majukumu yao ambayo waliyahaidi wakati wakiomba Ridhaa ya kuongoza kwani ni wajibu wao kuakikisha wanawatumikia wananchi ambao waliwaomba kura wakati wa kampeni.

No comments: