Wednesday, March 1, 2017

RC Makonda ahimiza usimamizi ujenzi wa barabara zenye viwango



MOSHI SHABANI MALLEMA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka wasimamizi wa miradi ya matengenezo ya barabara kuzingatia taaluma na weledi husika ili kupata thamani ya fedha kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu husika bila kukiuka taratibu za manunuzi.
RC Makonda ameyasema hayo alipokuwa anafungua kikao cha bodi ya barabara ya mkoa wa Dar es Salaam kilichofanyika katika ukumbi wa Arnautoglo na kuwaomba mameya, madiwani, wakuu wa wilaya na wakurugenzi kuifuatilia miradi hii kwa karibu, huku akishauri kuwa ni vyema miradi hii ikafanyika kwa gharama nafuu, kwa muda mfupi na kwa viwango, kwani fedha za wananchi ndiyo zinatumika wanapaswa kutendewa haki kwa kuona matokeo chanya kwenye miradi ya maendeleo.
Huku akisisitiza kuwa katika maslahi ya wananchi hatoangalia anagombana na wangapi, atahakikisha anatimiza wajibu wake.
Katika hatua nyingine kampuni ya ujenzi ya IBRA Contractors Limited kupitia Mkurugenzi wake Maida Waziri ameeleza kuhusu ujenzi wa barabara  zinazotumia teknolojia ya kisasa kwa udongo wa kawaida ni bora na huweza  kudumu zaidi ya miaka 10, haina vumbi wala uterezi na ujenzi wake hutumia muda mfupi na kuishauri serikali kutumia ujenzi huo wa gharama nafuu kwa takribani asilimia 50, huku akizitolea mfano Australia na Algeria kuanza kutumia ujenzi huo, hivyo hiyo ni suluhu ya lawama za muda mrefu kuhusu barabara mbovu nchini.
Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa ujenzi huo wa kibunifu utakuwa njia ya kuvifanya vijiji kuwa miji kupitia barabara.

Bwana Fabian Campagnolo kutoka kampuni ya ujenzi ya IBRA Contractors Limited , akitoa maelezo kwa wajumbe wa kikao hicho cha barabara , kuhusu ujenzi wa barabara zinazotumia teknolojia ya kisasa kwa udongo wa kawaida ni bora na huweza kudumu zaidi ya miaka 10, katika ukumbi wa Arnautoglo

No comments: