Thursday, February 23, 2017

KAMPUNI YA KUFUGA SUNGURA YA "THE RABBIT BLISS" SASA YAHAMIA DAR

 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Rabbit Blill inayohusika na ufugaji wa kisasa wa Sungura pamoja na uuzaji wake, Payas Ruben akizngumza na Ripota maalum wa Globu ya Jamii alietembelea makao makuu mapya ya Kampuni hiyo, yaliyopo eneo la Majohe, jijini Dar es salaam. Kampuni hiyo hivi sasa ipo Dar es salaam ikitokea Jijini Arusha kulikokuwa na makazi yake ya awali baada ya mmiliki wa sasa kununua hisa zote zilizokuwa zikimilikiwa na mmiliki wa awali. Akizungumza katika eneo hilo, Bw. Ruben alisema kuwa ufugaji wa Sungura ni mzuri sana na unafaida kubwa kwa mfugaji, kwani unaweza kumuingia kipato kikubwa kama atazingitia taratibu zote za ufugani, hivyo ametoa wito kwa wale wote wanaotaka kufuga au kujifunza ufugaji wa Sungura wasisite kufika kwenye ofisi zao zilizopo Majohe, Jijini Dar es salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Rabbit Blill inayohusika na ufugaji wa kisasa wa Sungura pamoja na uuzaji wake, Payas Ruben (kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mwena wa Kampuni hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Rabbit Republic ya nchini Kenya, Moses Mutua wakati wakimuangalia mmoja wa Sungura anaefugwa kisasa katika Shamba ya Sungura, lililopo Majohe, jijini Dar es salaam.

 Sehemu ya Mabanda ya kisasa kabisa ya kufugia Sungura.
 Baadhi ya Sungura wanaofugwa na Kampuni ya The Rabbit Blill.
 Moses Mutua a.k.a Mr. Rabbit akiwa kabeba mabox maalum ya Sungura wanaokuwa katika hali kuzaa.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya The Rabbit Blill wakiwa wamebeba baadhi ya Sungura wafugwao hapo.
Furaha ya kufuga Sungura kwa faida.

No comments: