Saturday, November 5, 2016

WATAALAM WA AFYA KUTOKA NCHI TISA AFRIKA WAPATIWA VYETI

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza katika mkutano wa wadau wa afya waliokutana Jijini Dar es Salaam Leo kwa ajili ya mafunzo ya kupima masikio na kuongea. Mafunzo hayo yamewawezesha washiriki kutoa huduma ya matibabu kwa watu wenye matatizo ya usikivu. Mafunzo hayo yameshirikisha wadau wa afya kutoka Nigeria Zambia, Ethiopia, Kenya, Malawi, Zimbabwe na Rwanda.
Baadhi ya washiriki kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wakimsikiliza Profesa Museru Leo.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya Koo, Sikio na Pua kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dr. Edwin Kayombo akifuatilia mkutano huo Leo.
Mtaalamu wa magonjwa ya Koo, Sikio na Pua akitoa mada kwenye mkutano huo Leo jijini Dar es Salam.
 
Mkurugenzi Mtendaji, Profesa Museru akikabidhi cheti kwa mmoja wa washiriki kutoka Muhimbili, JohnBosco Kambanga.
Mshiriki kutoka Rwanda, Fidel Munezero akipongezwa baada ya kukabidhiwa cheti Leo.
 
Wadau wa Afya wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mafunzo ya kupima masikio na kuongea yalioanza Oktoba 29, mwaka huu na kufungwa leo Novemba 5, 2016 jijini Dar es Salaam.Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

Watalaam 25 wa afya kutoka nchi tisa za Afrika leo wametunukiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo ya kupima masikio na kufundisha kuongea kwa watu wenye matatizo ya usikivu.

Mafunzo hayo yamewezeshwa na Kampuni ya MEDAL ya nchini Australia na kuhusisha washiriki kutoka nchi za Rwanda, Uganda ,Kenya , Zambia , Zimbabwe, Nigeria , Ghana, Malawi na Tanzania . Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ni mwenyeji wa mafunzo hayo.

Akikabidhi vyeti hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru ameishukuru Kampuni ya MEDAL kwa kuwezesha kutolewa kwa mafunzo hayo ambayo yanaisaidia Hospitali kupiga hatua katika mipango yake hususani katika suala la kutoa huduma kwa wale wenye matatizo ya usikivu.

Awali, Meneja wa Maendeleo Kanda ya Afrika Mohamed El Disouky amesema MEDEL wataendelea kushirikiana na wataalam mbalimbali wakiwemo wa Muhimbili ili kuhakikisha wanapata ujuzi wa kutosha katika kutoa huduma hiyo.

Mafunzo hayo yalianza Oktoba 29 mwaka huu jijini Dar es salaam na kumalizika Novemba 5, mwaka huu.

No comments: