Tuesday, November 15, 2016

TEA yatoa msaada wa vifaa vya TEHAMA Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika

 Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)  Bw. Joel Laurent (mweyesuti) alipotembelea chuo hicho kuangalia misaada ya vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano walivyovitoa chuoni hapo ikiwemo Ubao maalum za kufundishia (Smart Board) 4,Projecta 4 na Komputa 22, wa mwisho kulia ni Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bi. Sylvia Lupembe.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw. Joel Laurent akiongea na Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda(mwenye shati jeupe) ambapo alishauri kusimamia matumizi sahihi ya vifaa hivyo vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano vinatumika kwa manufaa ili kuleta matokeo yenye tija, mbele mwenye suti ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Dkt. Tumaini Katunzi na Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bi. Sylvia Lupembe.
 Makamu Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Dkt. Tumaini Katunzi na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw. Joel Laurent wakifuatilia maelekezo ya namna ubao maalum wa smart board unavyofanya kazi wakati wa kufundishia ikiwa ni moja ya msaada uliotolewa na mamlaka ya elimu.
 Sehemu ya Komputa 22 zilizotolewa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwenye chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC).
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)  Bw. Joel Laurent akiongea na wanafunzi wanaonufaika na msaada wa vifaa hivyo vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano vilitolewa katika Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC), Misaada mingine iliyotolewa ni Projecta 4 na Ubao maalum za kufundishia (Smart Board) 4.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)  Bw. Joel Laurent(kulia) akimkabidhi Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda moja ya projecta zitakazotumika katika kufundishia chuoni hapo, Misaada mingine ni Ubao maalum za kufundishia (Smart Board) 4 na Komputa 22.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)  Bw. Joel Laurent(kulia) akiwaeleza jambo Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda (katikati) na Makamu Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Dkt. Tumaini Katunzi (kulia) alipotembelea chuo hicho kuangalia misaada ya vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano walivyovitoa chuoni hapo.

No comments: