Friday, November 18, 2016

Taasisi ya Vijana ya TYVA na IRI Zatoa mafunzo kwa vijana kuhusu Mchakato wa mabadiliko ya katiba katika wilaya nne


Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania Bw, Deus Kibamba akitoa elimu kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba pamoja na historia ya mchakato huo kwa vijana wa wilaya ya Chamwino mkoani  Dodoma.
Afisa wa IRI, Tony Alfred akizungumza jambo wakakati wa mafunzo ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba kwa vijana wa wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
Makamu mwenyekiti wa TYVA, Kamala Dickson akizungumza jambo kwenye mkutano huo
Baadhi ya Vijana wa wilaya ya Chamwino wakiwa kwenye mafunzo kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba.

Katibu Mtendaji wa TYVA Saddam Khalfan akitoa ufafanuzi kuhusu shirika hilo wakati wa mafunzo hayo.
Baadhi ya Vijana wa wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mafunzo kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania Bw, Deus Kibamba akitoa elimu kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba pamoja na changamoto zake kwa vijana wa wilaya ya Tanga Mjini mkoani  Tanga.

Mmoja wa washiriki akichangia mada
Kijana mwenye ulemavu wa ngozi akisoma katiba ya Tanzania kwa makini sana wakati wa  mafunzo kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba yaliyofanyika Mjini Tanga.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo yaliyofanyika Tanga wakifuatilia mada

Na Mwandishi Wetu
Asasi Ya Vijana, Tanzania Youth Vision Association kwa Kushirikiana Na International Republican Institute zimetoa mafunzo ya kuboresha Uwezo wa Vijana kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba nchini katika Mikoa mitatu ilijumuisha Wilaya Nne, ikiwemo Kinondoni, Dodoma Mjini, Chamwino Na Tanga Mjini.

Mafunzo hayo yameweza kufikia vijana 500 kwa njia ya Warsha na Vijana aa wananchi zaidi ya 100,000 kupitia mitandao ya kijamii.

Lengo kuu la Mafunzo hayo ni kuongeza uelewa na ushiriki wa Vijana katika mchakato wa Mabadiliko ya Katiba. Katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Katibu Mtendaji wa TYVA ndugu Saddam Khalfan alisema, TYVA inaamini Katiba ni Sheria mama na mwongozo ambao una uhusiano wa moja kwa moja na maisha yetu ya kila siku.

Alibainisha watu wengi wamekua wakisoma au kuisikia Katiba, na wengine wakidhani Katiba ni maalumu kwa ajili ya wanasheria au wasomi tu. Kuna uhusiano mkubwa kati ya Katiba bora ya Nchi, Demokrasia na Maendeleo ya Jamii.

Mwanaharakati Na Mtetezi wa HAKI za Binadamu ndugu Deus Kibamba alipata kuwaelezea washiriki wa mafunzo hayo historia ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba, Ushiriki wa wananchi katika mchakato wa Katiba, hatua muhimu katika Mchakato wa utengenezaji Katiba, Mambo ya Msingi yaliyomo katika Katiba inayopendekezwa na Mambo muhimu kuelekea kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa.

Alidokeza pia, katika mchakato wa Katiba, hasa katika hatua ya Bunge la Katiba ulikosa maridhiano ya Kitaifa. kuna haja ya kuwepo mkutano wa kitaifa utajaowaleta wadau na jopo la wataalamu mbalimbali kwa ajili ya kunyambua yale mambo yanayoendelea kuleta ukakasi linapaswa kufanyika.

Ndugu Dickson Kamala ambaye ni Mtetezi wa HAKI za vijana na Makamu Mwenyekiti Wa TYVA aliwasilisha mada ya umuhimu wa Vijana kushiriki na  kushirikiana katika mchakato wa mabadiliko ya Katiba ili kupata Katiba itayojali maslahi yao na ya Taifa kwa ujumla.

Afisa kutoka IRI, Tony Alfred aliwatarifu Vijana washiriki kusoma kuhusu Katiba na wanaweza kupata habari na taarifa zaidi kuhusu Katiba kwa kupitia ujumbe mfupi wa maandishi kwa kutuma Neno "Katiba yetu" Kwenda 0684996494.

No comments: