Tuesday, November 1, 2016

RC PWANI AWATAKA WAJASIRIAMALI NCHINI KUWA WABUNIFU ILI KUWEZA KUSHINDANA KATIKA SOKA AFRIKA MASHARIKI

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo akiwahutubia wajasiriamali hawapo pichani wakati wa sherehe za ufungaji wa maonyesho ya tisa kanda ya mashariki yaliyofanyika katika viwanja vya mwanakalenge Wilayani Bagamoyo.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
mmoja wa wajasiriamali walioshiriki katika maonyesho ya tisa ya kanda ya mashariki yaliyofanyika katika viwanja vya mwanakalenge Wilayani Bgamoyo Jacob Luis akiwa katika gari yake ambayo ameitengeneza yeye mwenyewe ambapo mpaka kukamilika kwake ametumia gharama ya kiasi cha shilingi milioni tisa(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)

NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO 

WAJASIRIAMALI nchini wametakiwa kuhakikisha wanakuwa wabunifu na kutengeneza bidhaa zenye ubora wa kiwango cha juu ili kuweza kuleta ushindani na kuzipeleka katika soko la afrika mashariki ambalo lina idadi kubwa ya watu ili ziweze kuuzika na kukuza pato la Taifa.

Kauli hiyo imetolewa na MKUU wa Mkoa wa Pwani Injnia Evarist Ndikilo wakati wa sherehe za ufungaji wa maonyesho ya 9 ya wajasiriamali wadogo wadogo kutoka kanda ya mashariki yaliyofanyika katika viwanja vya Mwanakalenge Wilayani Bagamoyo.

Ndikilo alisema kwamba ili bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali wa Tannzania ziweze kuuzika katika soka la afrika mashariki kunahitajika juhudi za makusudi kutoka kw amamalaka ya chakula na dawa (TFDA) pamoja na Shirika la viwango Tanzania (TBS) kuzingatia maagizo waliyopatiwa na serikali wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo ili kuweza kukuza uchumi wa nchi.

Ndikilo akizungumzia kuhusina na changamoto inayowakabili wajasiriamali hao katika suala la upatikanaji wa vifungashio katika kuhifadhi bidhaa zao amesema kwamba serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya viwanda na biashara ipo tayari kutoa fungu la fedha kwa ajili ya kuweza kuwa na vifungashio hapa nchini kuliko kuviagizia kutoka nje ya nchi kwani ni gharama kubwa.

“Kwa upande wangu mimi napenda kuchukua fursa hii ya kuwaomba wajasiiamali kuwa wabunifu katika bidhaa ili kuweza kuleta ushindani mkubwa katika soka la afrika mashariki kwani kule ndio kuna idadi ya watu wengi zaidi kwa hivyo mkilizingatia hilo kutaweza kuleta mabadiliko chanya ya kuleta maendeleo,”alisema Ndikilo.

Aidha Ndikilo aliwataka wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wote nchini kuhakikisha wanatenga maeneo maaalumu kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vidogo vidogo na vikubwa ambayo vitaweza kusaidia kwa kisi kikubwa kuwapatia ajira vijana ambao wengi wao hawana kazi za kufanya.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika la viwanda vidogovidogo (SIDO) Tanzania Profesa Syvester Mpanduji alibanisha kwamba maonyesho hayo yameweza kuwapa fursa wajasiriamali kubadilishana ujuzi kupata mafunzo ikiwemo pamoja na kukuza uchumi wao kutokana na kuuza bidhaa zao .

Nao baadhi ya washiriki katika maonyesho hayo akiwemo Jacob Luis, Jania Omary pamoja na Rehema John walisema kwa sasa wanakabiliwa na chngamoto kubwa ya kutokuwa na vifungashio maalumu kwa ajii ya bidhaa zao hivyo wameimba serikali kupitia wizara ya viwanda na biashara kuwasaidia ili kuweza kufikia malengo yao.

MAONYESHO hayo ya kanda ya mashariki ambayo yamefungwa rasmi na mKuu wa Mkoa wa Pwani yameandaliwa na shirika la viwanda vidodovidogo (SIDO) Tanzania na yamewashirikisha wajasiriamali wadogo wadogo na wale wa kati zaidi ya 200 kutoka mikoa mitano ya Dar es Salaam, morogoro, Lindi, Mtwara , pamoja na wenyeji Mkoa wa Pwani .

No comments: