Friday, November 18, 2016

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO ATEMBELEA MNADA WA MHUNZE WILAYANI KISHAPU

Wafugaji wametakiwa kufuga kwa njia za kisasa kulingana na malisho badala ya kuwa na mifugo mingi huku wakikosa mahali pa kulishia.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, William Tate Ole Nasha alipotembelea mnada uliopo mjini Mhunze wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

Ole Nasha alisema si vyema wafugaji kuwa na mifugo mingi wakati hakuna rasilimali za kufugia kama nyasi ambazo katika maeneo mengi zipo chache hivyo kushindwa kukidhi mahitaji.Alisema pamoja na changamoto hizo Serikali kwa upande wake inaendelea na jitihada za kutatua changamoto hizo zinazowakabili wafugaji hapa nchini.

Aidha, Naibu waziri aliwataka wafanyabishara wa mifugo katika mnada wa Mhunze kujenga utamaduni wa kulipa ushuru wa Serikali badala ya kukwepa.Alisema kitengo cha kutorosha ng’ombe kukwepa kulipa ushuru wa mnada kunaikosesha Serikali mapato hivyo kushindwa kuwapa huduma.     
 Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, William Tate Ole Nasha (mwenye Kaunda suti ya bluu) akikagua ng’ombe ndani ya mnada wa Mhunze alipofanya ziara katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.
 Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, William Tate Ole Nasha akizungumza na wananchi katika viwanja vya mnadani alipozuru mnada mji mdogo wa mhunzewilayani Kishapu.
 Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, William Tate Ole Nasha (wa pili kulia) akifurahia jambo wakati mkutano wa hadhara katika viwanja vya mnadani. Wengine pichani kuanzia kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Boniphace Butondo, Katibu Tawala Wilaya, Shadrack Kangese na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga.
 Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi akiwasikiliza wafugaji na wafanyabiashara wa mifugo katika mnada wa Mhunze.
 Sehemu ya umati wa wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, William Tate Ole Nasha (hayupo pichani) wakati akiwahutubia viwanja vya mnadani.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Boniphace Butondo akizungumza katika mkutano huo wa hadhara.
Mkuu wa Idara ya Mifugo Wilaya ya Kishapu, Dk. Alphonce Bagambabyaki (kushoto) akitoa maelezo kuhusu mnada huo kwa ujumbe wa Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, William Tate Ole (wa pili kulia). Wengine pichani ni Leonard Basil kutoka Idara ya Uzalishaji na Masoko wizarani na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Stephen Magoiga (kulia).

No comments: