Sunday, November 13, 2016

Jamii yaaswa kufanya kazi kwa uaudilifu ili kujijengea heshima katika jamii

Katibu Mtendaji wa Baraza la Maaskofu  wa Katoliki Tanzania (TEC) Padre Raymond Saba akiwa katika picha ya pamoja na Dkt. Fredrick Kigadye wakati wa hafla ya kumkabidi tuzo mapema wikiendi hii Jijini Dar es Salaam.
Na Frank Shija, MAELEZO
Jamii imeaswa kufanya kazi kwa uadilifu, uaminifu, weledi na uzalendo wa hali ya juu ili wapate kuheshimika na kuthaminiwa na jamii zinazowazunguka kwa kutambua mchango wao katika kuendeleza jamii.
Hayo yamesemwa na Muadhama Kardinali Polycap Pengo wakati wa hafla ya kumkabidhi nishani ya Benemerenti  (Anayestahili), Dkt. Fredrick Kigadye, ambayo hutolewa na Baba Mtakatifu kwa mtu aliyetoa mchango mkubwa katika kulitumikia Kanisa na jamii kwa ujumla jana Jijini Dar es Salaam.
“Ni vyema tukatambua ya kwamba kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu ndiyo msingi mkuu wa mafanikio mahali pepote pa kazi na katika maisha yetu ya kila siku”. Alisema Kardinali Pengo.
Kwa upande wake Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Muashamu Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa masema kuwa Dkt. Kigadye amekuwa mtumishi wa wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kwa muda wa miaka 35 huku akifanya kazi katika Idara ya Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa mafanikio makubwa.
Ameonesha ni namna gani watu tunapaswa kujitoa kwa ajili ya kumtumikia Mungu kupitia vipawa na taaluma tulizo jaaliwakuwa nazo hii inatia moyo sana. Aliongeza Askofu Ngalekumtwa.
Akizungumzia Tuzo hiyo aliyopewa na Baba Mtakatifu Papa Francis, Dkt Kagadye amesema kuwa anajisikia mwenye furaha kubwa na wathamani kwa kupewa tuzo ya heshima na kiongozi mkubwa duniani nakuongeza kuwa tuzo hiyo inamuongezea chachu ya kuishi katika misingi imara ya maadili na weledi.
Aidha alitumia fursa hiyo kutoa raia kwa watanzania wengine hasa walei wa Kanisa Katoliki kutekeleza majukumu yao kwa kujituma zaidi ili kuwahudumia wana jamii wanaohitaji huduma za kanisa ikiwemo elimu, afya na nyingi nyingi. 
Dkt. Fredrick Kigadye amekuwa Mtanzania wa kwanza kutunukiwa tuzo hiyo baada ya  BABA Mtakatifu Fransisko kukubali maombi ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ya kumtunuku tuzo ya heshima aliyekuwa mkuu wa idara ya afya mstaafu wa Baraza hilo Dkt. Fredrick Kigadye kutokana na mchango mkubwa alioutoa kwa kanisa katoliki na baraza akiitumikia idara hiyo na majukuu mengine.
Tuzo hiyo 'BENEMERENTI' ilipokelewa kwa furaha na Katibu Mkuu wa TEC Padri Raymond Saba ambaye pamoja na kumpongeza Dkt. Kigadye, amesema watumishi wengine wa baraza lazima waige mfano wa utendaji wake.

Historia ya tuzo hiyo ilianzia miaka ya 1775 enzi za Papa Pius wa VI alipto watunuku tuzo ya Benemerenti wanajeshi waliokuwa wakitetea ukristu enzi hizo na baadaye mwaka 1925 ndipo ikaamuliwa kuwa tuzo hiyo itolewe kwa yeyote atakayekuwa ametoa mchango mkubwa kwa kanisa Katoliki na jamii kwa ujumla kupitia majukumu yake ya kazi za kila siku.

No comments: