Tuesday, November 29, 2016

ASILIMIA 40 YA WATANZANIA WAWE KWENYE UCHUMI WA VIWANDA KUFIKIA 2020


 WATANZANIA takribani asilimia 40 wanatakiwa wawe wamejiingiza kwenye uchumi wa viwanda mpaka kufikia 2020 ili kuweza kusaidia kukuza ajira za vijana na kuifanya Tanzania kuwa kwenye uchumi wa kati kwa maendeleo ya jamii na nchi kwa ujumla. 

 Akizungumza hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa nne wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa msimbomilia (Barcode) za bidhaa (GS1) Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage amesema kuwa Serikali imeazimia kufikisha asilimia 40 ya watanzania kufanya shughuli za uchumi wa viwanda kufikia 2020.

 “Tunataka mpaka kufikia 2020 watanzania takribani asilimia 40 wawe wamejikita kwenye uchumi wa viwanda ili kusaidia kukuza ajira kwa vijana na kuifanya Tanzania kuwa kwenye uchumi wa kati kwa maendeleo ya jamii nan chi yetu kwa ujumla” alisema Waziri Mwijage.

 Aidha Waziri Mwijage amesema kuwa Uchumi wa viwanda unatakiwa kukua nchini kuwezesha kuzalisha bidhaa bora zitakazouzwa ndani na nje ya nchi ili kukusanya kodi kwa ajili ya kupata huduma bora za kijamii kwa maendeleo ya wananchi wa Tanzania . 

 Kwa upande wa Afisa Mkuu wa elimu kwa mlipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) ambao ni wadhamini wa mkutano huo Bi. Rose Mahendeka alisema kuwa wafanya biashara wote ambao wanahitaji kutumia mfumo wa kuuza bidhaa kwa kuweka msimbomilia(Barcode) wanapaswa kupitia TRA kwa ajili ya usajili na uhakiki wa namba ya utambulisho ya mlipa kodi(TIN) kabla ya kwenda kupata huduma ya msimbomilia.

 “Wafanya biashara wote ambao wanahitaji kutumia mfumo wa kuuza bidhaa kwa kuweka msimbomilia(Barcode) wanapaswa kupitia TRA kwa ajili ya usajili na uhakiki wa namba ya utambulisho ya mlipa kodi(TIN) kabla ya kwenda kupata huduma” alisisitiza Bi. Mahendeka. Aidha Bi. 
Mahendeka alisema kuwa wafanya biashara ambao wanahitaji kuuza bidhaa zao kwa kutumia msimbomilia wanapasa kulipa kodi bila ya kukwepa ili kuwezesha Tanzania kupiga hatua kufikia uchumi wa viwanda ili kupata huduma bora kwa maendeleo ya jamii.

 Naye Mwenyekiti wa bodi ya GS1 Bw. Gideon Mazara amesema kuwa wafanyabiashara wanatakiwa kutumia msimbomilia wa Tanzania ili kuweza kutangaza bidhaa za nchini ili kuweza kupata soko la kimataifa na kufikia uchumi wa kati . 

 “Ni lazima kutumia msimbomilia wa Tanzania kwa kila mfanyabiashara na mjasiriamali ili kuweza kutangaza bidhaa za nchini ili kuweza kupata soko la kimataifa na kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda vikubwa na vidogo” alisema Bw. Mazara.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage akiongea na wadau mbalimbali wa biashara kuhusu umuhimu wa kulipa kodi na kutumia msimbomilia(barcode) hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa nne wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa msimbomilia (Barcode) za bidhaa (GS1) uliofanyika jijini dar es salaam.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage wa pili kulia akikata keki kuadhimisha mwaka wa nne wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa msimbomilia (Barcode) za bidhaa (GS1) uliofanyika jijini dar es salaam wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya GS1 Bw. Gideon Mazara.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage kulia akimpa mkono wa pongezi Afisa Mkuu wa elimu kwa mlipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kwa kudhamini mkutano wa mwaka wa nne wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa msimbomilia (Barcode) za bidhaa (GS1) uliofanyika jijini Dar es salaam.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage kushoto akipokea zawadi kutoka kwa mwakilishi wa kampuni ya Shea illushion kulia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa nne wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa msimbomilia (Barcode) za bidhaa (GS1) uliofanyika jijini dar es salaam. Na Mpiga picha Wetu . Dar es salaam.

No comments: