Saturday, October 22, 2016

YANGA WAIADHIBU KAGERA SUGAR BAO 6-2 KWENYE UWANJA WA KAITABA MJINI BUKOBA LEO

Yanga leo wameichakaza Kagera Sugar 6-2 kwenye Mechi ya VPL, Ligi Kuu Vodacom, ilityochezwa huko Uwanja wa Kaitaba, Bukoba na kuchupa hadi Nafasi ya Pili.
Kagera Sugar ndio waliotangulia kupata Bao katika Dakika ya 3 Mfungaji akiwa Mbaraka Yusuf na Yanga kusawazisha Dakika ya 4 kupitia Straika wao kutoka Zimbabwe Donald Ngoma.
Yanga walipa Bao la Pili Dakika 21 kupitia Simon Msuva na Straika wa Zambia, Obrey Chirwa, kuipa Bao la 3 Dakika ya 26.
Yanga waliongoza kwa Bao hizo 3 hadi Mapumziko.
Kipindi cha Pili, Dakika ya 49, Mbaraka Yusuf, kwa mara ya pili, akaipa Kagera Sugar Bao lao la Pili lakini Yanga wakaja juu na kupiga Bao 3 nyingine katika Dakika za 58, 63 na 64 kupitia Deus Kaseke, Chirwa na Ngoma.
Timu ya Pili ni Yanga yenye Pointi 21 kwa Mechi 10 wakifungana na Stand United, waliocheza Mechi 12, lakini wana udhaifu wa Magoli na hivyo kushika Nafasi ya 3.
Jumapili Oktoba 23 zipo Mechi 2 wakati Simba watakapocheza na Toto Africans ya Mwanza Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na huko Sokoine, Mbeya ni kati ya Tanzania Prisons na Mbao FC.

Waamuzi wa Mtanange uliochezwa leo hii kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba Kagera Sugar Dhidi ya Timu ya jijini Dar es Salaam Yanga.

Viongozi walisalimiana kabla ya kipute kuanza, Picha Zote na Faustine Ruta. Bukoba

Kikosi cha Yanga kilichoanza

Kikosi cha Kagera Sugar kilichoanza

Picha ya pamoja

Ngoma aliisawazishia bao Yanga mapema kipindi cha kwanza

Taswira mtanage ukiendelea
Mchezo huo umezalisha mabao nane ambapo Casillas alifungwa mabao matatu mepesi katika dakika 27 pekee alizokuwa langoni kabla ya Kocha Mecky Mexime kumtoa na kumuingiza David Burhan ambaye nae alifungwa matatu.
Cassilas alishindwa kujiamini langoni ambapo alifanya makosa kadhaa katika dakika chache alizodumu uwanjani ambapo kama washambuliaji wa Yanga wangeongeza umakini kabla ya mlinda mlango huyo kufanyiwa mabadiliko basi wangeweza kufunga zaidi ya mabao hayo kipindi cha kwanza.
Washambuliaji Obrey Chirwa na Donald Ngoma walifunga mabao mawili kila mmoja huku Simon Msuva na Deus Kaseke wakifunga moja moja na kukamilisha karamu hiyo ya mabao.






Shangwe...


















Furaha kwa ocha mkuu wa Yanga SC, Hans van Der Pluijm baada ya kuona Timu yake ikiinyeshea mvua ya mabao Timu ya Kagera Sukari.

No comments: