Saturday, October 22, 2016

WAZIRI KAIRUKI AMALIZA ZIARA YA SIKU 2, KUWATEMBELEA, KUWASIKILIZA NA KUZUNGUMZA NA WANUFAIKA TASAF WA MANISPAA ZA KINONDONI NA TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, akipokewa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva, alipowasili Ofisi za mkuu huyo jana kwa ajili ya kuhitimisha ziara yake ya siku mbili kuwatembelea, kuwasikiliza na kuzungumza na wanufaika hao wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf ) wa Manispaa za Kinondoni na Temeke jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf ) na wakazi wa maeneo ya Sandali, wakiwa katika mkutano na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, kwenye Mtaa wa Mamboleo, Manispaa ya Temeke, jijini Dar es Salaam jana. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Diwani wa Kata ya Sandali, Temeke jijini, Abel Tarimo, akitoa maelezo kuhusu masuala mbalimbali kwenye mtaa wake huo, kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, alipokuwa na mkutano na wanufaika wa Tasaf pamoja na wakazi wa maeneo hayo jana.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva, akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki (kulia), kuzungumza na wanufaika wa Tasaf pamoja na wananchi ambao kaya zao hazijaingizwa katika mpango huo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Nasib Mbaga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, akizungumza na wanufaika wa Tasaf pamoja na wananchi wa Kata ya Sandali, ambao kaya zao bado hazijaingizwa katika mpango huo. 
Baadhi ya watendaji wa Mkoa na waratibu wa Tasaf wa Manispaa ya Temeke wakiwa katika mkutano huo, wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, wakati alipokuwa akizungumza na wanufaika wa Tasaf pamoja na wananchi ambao kaya zao bado hazijaingizwa katika mpango huo. 
Baadhi ya waratibu wa Tasaf wa Manispaa ya Temeke wakiwa katika mkutano huo. 
Mmoja wa wanufaika wa Tasaf, akimpatia zawadi ya kitenge Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki (kulia), baada ya kuzitumia fedha za ruzuku anazopewa na Tasaf katika mradi wa kutengeneza bidhaa hizo. 
Naibu Meya wa Manispaa ya Temeke, Feysal Salum, akizungumza na wanufaika pamoja na wananchi ambao hawajanufaika na Tasaf, wakati wa mkutano huo, Mtaa wa Mamboleo, Kata ya Sandali jijini Dar es Saaam.
Diwani wa Kata ya Mtoni, Benard Mwakyembe, akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, alipofika na kufanya mkutano na wanufaika wa Tasaf pamoja na wananchi ambao bado hawajaingizwa katika mpango huo, maeneo ya Shule ya Msingi Mtoni, jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya wanufaika wa Tasaf katika mpango wa Serikali wa kuzinusuru kaya masikini pamoja na wananchi ambao bado hawajaingizwa katika mpango huo wa maeneo ya Kata ya Mtoni, Temeke jijini Dar es Salaam jana, wakisikiliza masuala mbalimbali yaliyokuwa yakielezwa katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Uratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf), Alphonce Kyariga, akitoa ufafanuzi katika kuwapa ufahamu wanufaika wa Tasaf pamoja na wananchi wa maeneo hayo ya Kata ya Mtoni, ambao bado hawajaingizwa katika mpango huo wa kunusuru kaya masikini. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki.
Mmoja wa wananchi wa Kata ya Mtoni, ambaye bado kaya yake haijaingizwa katika mpango huo, Rajab Bakari, akitoa malalamiko yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki kuhusu kutokufikiwa na mpango huo, ilhali akiwa ni mmoja wa watu wanaostahiki kupata ruzuku hiyo.
Mwananchi wa Kata ya Mtoni, ambaye bado kaya yake haijaingizwa katika mpango huo, Uwesu Thabiti, akitoa malalamiko yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki kuhusu kutokufikiwa na mpango huo, ilhali akiwa ni mmoja wa watu wanaostahiki kupata ruzuku hiyo.

No comments: