Monday, October 31, 2016

OLIVE Kiarie kutoka Kenya aibuka mshindi wa Maisha Plus East Africa 2016

Olive Kiarie, mshiriki kutoka nchini Kenya ameibuka mshindi wa Maisha Plus East Africa 2016 na kujishindia kitita cha Tzshs. Milioni 30. “Kwanza napenda kumshukuru Mungu. Nimetoka Kenya kuja kutafuta hii pesa na nimeipata, hivyo namshukuru Mungu. Nawashukuru mabeste wangu wote, na wote walionipa sapoti. Asante pia Babu.” Alisema Olive huku akitoka machozi baada ya kutangazwa mshindi. Hii ni mara ya kwanza kwa taji hilo kwenda nje ya Tanzania ikiwa ni msimu wa tano toka mashindano haya yaanze mwaka 2009. Olive anakua msichana wa pili kujishindia taji hilo baada ya Bernick Kimiro aliyeshinda mwaka 2012.



Hivi ndivyo ilivyokua pale OLIVE KIARIE alipotangazwa mshindi wa Maisha Plus East Africa 2016. #VijanaNdioNgazi #HapaKaziTu


A video posted by Maisha Plus (@maishaplus) on Oct 30, 2016 at 10:19pm PDT
Add caption

Shindano la Maisha Plus lilijumuisha washiriki 30 kutoka nchi tano za Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda ambapo washiriki 16 tu ndio waliofanikiwa kuingia fainali. Washiriki Aloyce Sambuta, Irene Ishengoma, Alex Essau, Ngenda Pilly, Nibigira Baswari, Grace Pemba, Denaice Machocho, Umubyeyi Solange, Assimwe Marvin, Salmin Omary, Rukia Athuman, Mike Curtywer, Yasinta Mrisho, Karekezi Jean na Namita Cherrie walifanikiwa kuingia fainali ambazo zilirushwa jana usiku na kituo cha televisheni cha Azam Two. [caption id="attachment_148" align="alignnone" width="742"] Washiriki walioingia Top 5 ya Maisha Plus kutoka kushoto: Aloyce Sambuta, Alex Essau, Olive Kiarie, Irene Ishengoma na Ngenda Pilly.[/caption] Katika hatua nyingine washiriki wanne walipewa tuzo. Aloyce Sambuta alipata tuzo ya Rais bora na kupewa jumla ya Tshs.Laki nne, Ngenda Pili alipata tuzo ya mshiriki mwenye heshima kubwa, Mike Cutywer alipaza tuzo ya mshiriki mdogo wa kiume wakati Namita Cherrie alipata tuzo ya mshiriki mdogo wa kike. [caption id="attachment_150" align="alignnone" width="742"] Top 3 ya Maisha Plus Aloyce Sambuta, Olive Kiarie na Irene Ishongoma, Wasanii Ommy Dimpoz na Joh Makini walitoa burudani wakati wa fainali hizo. 880A9978880A0043880A0055   880A0125880A0127880A0129880A0130880A0132880A0134880A0166880A0169880A0172880A0184880A0210

No comments: