Thursday, October 27, 2016

MSEMAJI WA SERIKALI: TUTAIMARISHA UHUSIANO NA USHIRIKIANO NA VYOMBO VYA HABARI NCHINI

ef1
Mhariri Mkuu wa kituo cha redio cha EFM Radio cha Jijini Dar es Salaam, Scholastica Mazula akisalimiana na Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas wakati wa ziara yake ya kutembelea ofisi za kituo hicho leo Jijini humo kwa ajili ya kubadilishana mawazo na uzoefu wa kazi.
ef2
Mhariri Mkuu wa kituo cha redio cha EFM Radio cha Jijini Dar es Salaam, Scholastica Mazula akitoa ufafanuzi kwa Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas wakati wa ziara yake ya kutembelea ofisi za redio hiyo leo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kubadilishana mawazo na uzoefu wa kazi. Kulia ni Mtangazaji wa redio hiyo, Boneventure Kilosa.
ef3
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akiwa katika picha ya pamoja na Mtangazaji wa kipindi cha michezo cha redio ya EFM, Ibrahim Masoud “Maestro” wakati wa ziara yake ya kutembelea ofisi za kituo hicho leo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kubadilishana mawazo na uzoefu wa kazi.
ef4
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas (mwenye suti) akiwa katika picha ya pamoja na Mtangazaji wa kipindi cha Ubaoni kinachorushwa hewani na kituo cha redio ya EFM,  Silvester Mjuni   (kushoto) wakati wa ziara yake ya kutembelea ofisi za kituo hicho leo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kubadilishana mawazo na uzoefu wa kazi. Wengine kushoto ni Afisa Habari Mwandamizi wa Idara ya Habari Jonas Kamaleki na Afisa Habari Beatrice Lyimo.
ef5
Mtangazaji wa kipindi cha UBAONI kinachorushwa hewani na kituo cha redio cha cha EFM cha Jijini Dar es Salaam, Silvester Mjuni (katikati) akiendesha mahojiano maalum ya kipindi hicho na Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas (kushoto) wakati wa ziara yake ya kutembelea ofisi za kituo hicho kwa ajili ya kubadilishana mawazo na uzoefu wa kazi. Kulia ni Afisa Habari(MAELEZO), Jonas Kamaleki.
ef6
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akizungumza katika mahojiano maalum ya kipindi cha cha UBAONI kinachorushwa hewani na kituo cha redio cha EFM redio cha Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari Mwandamizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Jonas Kamaleki.
(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA -MAELEZO)



SERIKALI imeahidi kuendeleza uhusiano na ushirikiano na vyombo vya habari nchini ili kuviwezesha kutelekeleza vyema wajibu wake kwa umma.

Akizungumza katika wakati tofauti wakati wa ziara yake ya kutembelea taasisi za Vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Habari Hassan Abbas alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vinakuwa chachu ya maendeleo ya wananchi nchini.

Aliongeza kuwa yapo mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na Serikali katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo umeme, maji, barabara, afya, elimu, ambapo taarifa za utekelezaji wa ahadi hizo za Serikali hazijaweza kuandikwa na kutangazwa na vyombo vya habari.

Abbas alisema katika kuimarisha mfumo wa utoaji wa habari na taarifa kwa umma, ofisi yake kwa kushirikiana na Shirika la Utangazaji nchini (TBC) wameanzisha kipindi cha TUNATEKELEZA ambacho kinatoa fursa kwa Viongozi wa Serikali kutoa taarifa kwa umma kuhusu utelekezaji wa mipango mbalimbali ya Serikali.

Aidha Abbasalisema ofisi yake ndiye msimamizi na mratibu mkuu wa vitengo vya mawasiliano Serikali, hivyo alitoa wito kwa wanahabari kuwasiliana naye mara kwa mara pindi wanapokabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa taarifa katika ofisi za umma.

Kuhusu mafunzo kwa wanahabari, Abbas alivitaka vyombo vya habari kutumia fursa ya waandishi wakongwe waliopo katika ofisi zao, ambao wamebobea katika maeneo mbalimbaloi ikiwemo uandishi wa makala, habari na upigaji picha.

Kwa mujibu wa Abbas alisema kwa sasa, ofisi yake inaendelea na zoezi la kuwahamasisha Maafisa Habari wa Serikali katika Wizara, Idara, Taasisi, Wakala, Mikoa, na Wilaya nchini kuanza mageuzi katika mfumo wa taarifa kwa umma ikiwemo kutumia mitandao ya kijamii.

No comments: