Monday, October 3, 2016

MPIGA CHAPA MKUU WA SERIKALI AMKABIDHI MHE. JAJI MKUU BENDERA YA TAIFA NA YA AFRIKA MASHARIKI.

Mpicha Chapa Mkuu wa Serikali, Kassian Chibogoyo akizungumza na Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman kabla ya kumkabidhi Bendera ya Taifa na Ile ya Afdrika Mashariki leo katika Ofisi ya Jaji Mkuu jijini Dar es salaam.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akikabidhiwa Bendera ya Taifa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Kassian Chibogoyo  leo ofisini kwake jijini Dar salaam.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akikabidhiwa Bendera ya Afrika Mashariki na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Kassian Chibogoyo  leo ofisini kwake jijini Dar salaam.
  Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akifurahia Zawadi ya Tai ya Bendera ya Taifa aliyopewa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Kassian Chibogoyo  leo ofisini kwake jijini Dar salaam.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akimwonyesha Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali kitabu cha Sheria kuhusu matumizi ya Vielelezo vya Taifa kabla ya kukabidhiwa Bendera ya Taifa na ile ya Afrika Mashariki.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo pichani) kabla ya kukabidhiwa  Bendera ya Taifa na ile ya Afrika Mashariki na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Kassian Chibogoyo  ofisini kwake leo jijini Dar salaam. 

Na Mary Gwera, MAHAKAMA
JAJI Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman amezitaka Wizara, Halmashauri na Taasisi nyingine za Serikali kutumia vielelezo vya Taifa kama bendera na nembo ya taifa katika ofisi zao ili kuenzi tunu na vielelezo vya Taifa.

Aliyasema hayo ofisini kwake Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam alipokuwa akipokea rasmi bendera ya Taifa na Afrika Mashariki kutoka kwa Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Bw. Cassian Chibogoyo.

Alisema kuwa  vielelezo hivi vya taifa vinalindwa kisheria kwa hiyo inabidi vipate heshima yake kwa kuwa vinawakilisha taifa.

“Sheria pia inavitambua vielelezo hivi hivyo ni muhimu vikapewa heshima yake, kwani hata mtu akichezea vitu hivi anaweza kufungwa kwa mujibu ya sheria,” alisisitiza Jaji Mkuu.

Aliongeza pia Mahakama ya Tanzania pia iko katika mchakato wa kupata bendera yake kama ilivyo kwa Taasisi nyingine kama Bunge, pamoja na nembo yake ili ziweze kutumika katika Mahakam azote nchini.

Awali; akiongea na Jaji Mkuu pamoja na waandishi wa habari kabla ya makabidhiano hayo, Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Bw. Cassian Chibogoyo pia alizitaka Taasisi za Serikali kutopuuzia umuhimu wa matumizi wa vielelezo vya Taifa.

Alisema kuwa baadhi ya Ofisi nyeti za Serikali hazina bendera na vielelezo vingine muhimu ambavyo vinaiwakilisha Taifa na kusisitiza matumizi yake ili kuenzi tunu za Taifa.

“Ofisi nyingi za Serikali zinatumia bendera zilizochakaa na nyingine hazina kabisa, vitu hivi ni muhimu kwa taifa hivyo ni vyema kuvienzi na kuvithamini pamoja na kuvitunza,” alisema Bw. Chibogoyo.

No comments: