Friday, October 14, 2016

Dk.Kigwangalla na Mwigulu Nchemba waombewa dua na Sheikh Mkuu wa jumuiya ya Bohora Duniani

Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla jioni hii ya leo Oktoba 13.2016 amekaribishwa na dhehebu la Bohora na kuombewa dua maalum na Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin katika msikiti wa dhehebu hilo Upanga Jijini Dar es Salaam.

Mbali na kutoa dua kwa Dk. Kigwangalla, Sheikh Dkt. Syedna ameahidi kuleta wawekezaji wa Kibohora kutoka sehemu mbalimbali Duniani kwa ajili ya kuwekeza kwenye ujenzi wa Mahospitali ikiwemo Hospitali za Rufaa za kisasa pamoja na Viwanda vya Dawa hali ambayo itapunguza idadi ya wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa ajili ya kufuata matibabu.

Pia viwanda vya dawa vitashusha gharama za dawa nchini na kupunguza ucheleweshaji unaosababishwa na kuagiza dawa nje ya nchi.

Aidha, katika tukio hilo, usiku huu, Dk.Kigwangalla ameweza kushuhudia ndoa za Vijana zaidi ya 50 zikifungishwa na Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna.

Mbali na Dk.Kigwangalla kuombewa dua maalum na Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna, Mbunge wa Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mh. Mwigulu Nchemba aliungana katika kuombewa na Shehe huyo.
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa na Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin (kulia) wakati wa kuombewa dua maalum usiku huu.
Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin (kulia) akimuombea Dua maalum Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto aliyefumba macho)
Dua zikiendelea
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akibusu mkono wa Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin isharara ya kupokea dua katika tukio hilo
Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin akimuaga Dk.Kigwangalla baada ya dua

Mbunge wa Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mh. Mwigulu Nchemba akiombewa dua katika tukio hilo.
Watu kutoka Mataifa mbalimbali Duania ikiwemo jamii ya Bohora ambao pia wapo hapa nchini nao wamepata bahati ya kuombewa dua maalum na Shehe huyo Mkuu
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoka katika tukio hilo la kuombewa dua
Mbunge wa Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mh. Mwigulu Nchemba akitoka katika tukio hilo la kuombewa dua 
Mbunge wa Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mh. Mwigulu Nchemba akisalimiana na Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla wakati wa tukio hilo
Picha ya pamoja 
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akipata picha pamoja baadhi ya vijana ambao walipata kufunga ndoa na wake zao ndoa ambazo zaidi ya 50 zimefungwa huku Shehe Mkuu huyo wa Mabohora Duniani pia alipata kuzibariki.

No comments: