Sunday, September 18, 2016

SERENGETI BOYS YAIBURUZA CONGO BRAZZAVILLE 3-2 UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR LEO

 Ankal na mtangazaji Mkongwe Abdallah Majura walikuwepo kushuhudia  Serengeti Boys wakicheza dhidi ya Congo Brazaville wa kuwania kufuzu kucheza katika Mashindano ya Kombe la Afrika la Vijana chini ya Miaka 17, yatakayofanyika Nchini Madagascer mwakani. Nyuma yao ni Kanali Mstaafu Iddi Kipingu
Mbunge wa Jimbo la Kiembe Samaki Mh.Ibrahim Raza na familia yake walikuwepo pia 
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye  na wadau wa michezo wakiwa jukwaa juu.
 Kocha wa Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa "Master" akiangalia madini mapya
 Mmoja wa viongozi wa timu ya Congo Brazaville akishangilia 
 Ankal akiwa na mweka hazina msaidizi wa Kariakoo Family Development Foundation (KFDF) uwanjani
 Timu zikiwa uwanjani kabla ya mchezo
 Wimbo wa Taifa
 Furaha ya ushindi
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wachezaji wa Serengeti Boys na waandishi wa habari  Jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa mechi yao dhidi ya Congo-Brazaville 
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Vijana "Serengeti Boys", Yohana Oscar Mkomola akikimbilia upande walipo mashabiki mara baada ya kuipatia timu yake Goli, katika Mchezo wao dhidi ya Congo Brazaville wa kuwania kufuzu kucheza katika Mashindano ya Kombe la Afrika la Vijana chini ya Miaka 17, yatakayofanyika Nchini Madagascer mwakani. Serengeti Boys imeibuka na ushishi mwembamba wa bao 3-2, hivyo watajipanga kwa mchezo wa marudiano utakaochezwa juma lijalo. Magoli ya Serengeti Boys yamefungwa na Yohana Oscar dakika ya 38 na 42 na Issa Abdi Makamba dakika ya 70, huku magoli ya Congo Brazaville yakifungwa na Langa-Lesse Percy kwa mkwaju wa penani na dakika ya 90 Poboumela Chardon. 

Shambulizi la hatari langoni mwa Timu ya Serengeti Boys.Mchezaji wa timu ya Serengeti Boys,Yohana Oscar Mkomola akitoka mbio maara baada ya kuachia mkwaju mkali kwa golikipa wa timu ya Congo Brazaville,na kutinga wavuni,likiwa ni goli la pili mnamo dakika ya 42 kipindi cha kwanza.
Mabeki wa Timu ya Congo Brazaville wakiusindikiza kwa macho mpira uliopigwa vizuri kabisa na Mchezaji wa Serengeti Boys, Issa Abdi Makamba na kuipatia timu yake bao la tatu, katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza katika Mashindano ya Kombe la Afrika la Vijana chini ya Miaka 17, yatakayofanyika Nchini Madagascer mwakani.
Beki wa Timu ya Taifa ya vijana ya Congo Brazaville, Moundza Prince akiwa ameruka juu kuondosha hatari iliyokuwa imeelekeswa langoni kwake, katika mchezo dhidi ya Serengeti Boys uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam.
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Vijana "Serengeti Boys", Asad Juma akichuana vikali na Mpinzani wake Mboungou Prestige wa Timu ya Congo Brazaville, katika mchezo dhidi ya Serengeti Boys uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam.
 Shangwe za mashabiki wa Serengeti Boys.
Ankal na Wadau wakifatilia Mchezo huo.

Mchezaji wa timu ya Congo Brazzaville Ngumbi Exau akiruka hewani kumzuia mchezaji wa timu ya Serengeti Boys Yohana Oscar Mkomola asiondoke na mpira.
Katika kipindi cha kwanza kila timu zilionesha kiu kubwa ya kutaka kupata magoli mapema,kila timu ilikuwa ikishambulia lango la mwenzake kwa spidi kubwa,mpaka dakika 90 za mchezo timu ya Serengeti Boys imeibuka kwa ushindi wa goli 3-2 dhidi ya Congo Brazzavile.
 


BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

No comments: