Saturday, September 17, 2016

DC ILALA,SOPHIA MJEMA AONGOZA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUCHANGIA WAATHIRIWA NA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA


1
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akipokea kiasi cha shilingi milioni zaidi ya milioni 6 kutoka kwa mmoja wa wafanyabiashara wa Kariakoo Bw. Deo Senya wakati Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo (JWK) walipofanya Harambee ya kuchangia wahanga wa Tetemeko la Ardhi kule Bukoba mkoani Kagera ambapo Mkuu wa wilaya hiyo aliongoza harambee hiyo, Kuliani ni Katibu Tawala wa wilaya ya Ilala Bw. Edward Mpogolo na katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanya Biashara Kariakoo Bw.Philimin Lomano Chonde.

Katika harambee hiyo jumla ya shilingi milioni 13,708,000/= fedha taslimu zilikusanywa na vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 31564800/= jumla ya michango kwa ujumla ni shilingi milioni 45,672,800/= harambee hiyo leo ilikuwa inazinduliwa rasmi na michango inaendelea mpaka siku ya jumamosi ijayo ambapo ndiyo harambee hiyo itafungwa rasmi na wafanyabiashara mbalimbali wametakiwa kuendelea kuchangia kwa kupitia jumuiya yao ya wafanyabiashara mpaka siku ya jumamosi.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
2
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akipokeamsaada wa viatu kutoka kwa wafanyabiashara wa kikundi cha Raha Square wafanyabiashara ambao wametoa mchango ubwa sana wa fedha na vitu mbalimbali katika harambee hiyo.
3
Wafanyabiashara wa Raha Square Kariakoo wakikabidhi mcahngo wao wa fedha kwa mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema.
4
Raha Square wakikabidhi Magodoro , Nguo, Vikoi , Mashuka na vitu vingine mbalimbali katika harambee hiyo.
5 6
Wakikabidhi Suti na vitengi pamoja na mashuka katika harambee hiyo.
7
Mkuu wa wilaya ya Ilala akipiga picha ya pamoja na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo mara baada ya harambee hiyo.
8 9
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akiwahutubia wafanyabiashara na wananchi mbalimbali waliohudhuria katika harambee hiyo.
10
Mfanyabiashara Mohammed Abdallah Nofa akizungumza mara baada ya kukabidhi mchango wake wa shilingi 500.000 kwa Mkuu wa wilaya Ilala Mh. Sophia Mjema wa pili kutoka kulia . katika picha kulia ni Edward Mpogolo Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala na Kushoto ni Katibu wa JWK Bw. Abdallah Mwinyi
11
Wafanyabiashara kutoka Raha Square wakikusanya michango yao ya fedha taslimu na vifaa mbalimbali kabla ya kuvikabidhi leo.
12
Kiongozi wa Wafanyabiashara wauza Simu za mkononi Bw.Stanley Mwakipesile akizungumza machache mara baada ya kukabidhi mchango wao zaidi shilingi milioni 1.500.000 kwa mkuu wa wilaya ya Ilala katika Harambee hiyo.

No comments: