Monday, August 8, 2016

VIONGOZI WA SERIKALI NA WANANCHI WAFURAHIA HUDUMA ZA MIFUKO YA UWEKEZAJI WA PAMOJA YA UTT AMIS

Waziri wa Fedha Dr.Philip Mpango (Kushoto) akisalimiana na Bw. Simon Migangala Kaimu Mkurugenzi mkuu UTT AMIS wakati alipotembelea banda la wizara ya fedha katika viwanja vya NaneNane Ngongo mkoani Lindi. 
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi akipata maelezo ya kina kuhusiana na mifuko ya uwekezajiwa pamoja inayoendeshwa na UTT AMIS.Kushoto ni Afisa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS Bw. Rahim Mwanga akitoa Maelezo hayo. 
Bi. Surah Twaakyondo, Afisa kutoka UTT-AMIS akitoa maelezo ya jinsi ya kuwekeza kwenye Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja kwa wananchi waliotembelea banda wakati wa maonyesho ya NaneNane yaliyofanyika kitaifa mkoani Lindi. 
Bi Ashura Kassim wa UTT AMIS akiwasaidia wananchi wa mkoa wa Arusha kujiunga katika uwekezaji wa pamoja 
Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya uwekezaji ya UTT AMIS ndugu Daudi Mbaga akitoa elimu kwa wananchi kwenye viwanja vya Nane Nane Arusha. 
Ni furaha iliyoje kuwekeza na UTT AMIS ..mteja Nane Nane Arusha baada ya kujiunga na UTT AMIS

UTT AMIS ni kampuni inayoendesha mifuko ya uwekezaji wa pamoja hapa nchini. Mpaka sasa inaendesha mifuko mitano ambayo ni Mfuko wa Umoja, Mfuko wa Wekeza Maisha, Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Kujikimu na Mfuko wa Ukwasi yenye jumla ya thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 253. 

Mifuko ya uwekezaji wa pamoja ni fursa mbadala inayowezasha watu ,vikundi,taasisi na kampuni sawa na mahitaji yao kuwekeza pesa zao kwa meneja wa mfuko(UTT AMIS) kisha meneja huwekeza fedha hizo katika masoko ya fedha na masoko ya mitaji kulingana na waraka wa makubaliano. Faida ipatikanayo hugawanywa kwa wawekezaji kulingana na uwiano wa uwekezaji waliofanya katika mfuko husika. 

Mifuko yote hii imeweza kukidhi vigezo muhimu vya uwekezaji ambavyo ni Usalama,Ukwasi na Faida (Safety, Liquidity and Returns). Wawekezaji wote wananufaika kwa kupata faida shindani hivyo kuweza kukuza mitaji yao, uwekezaji mseto hufanyika ili kupunguza hatari za uwekezaji,utalaamu wa meneja wa mifuko,unafuu mkubwa wa gharama na uwazi ni vichocheo vinavyofanya UTT AMIS kuwa kimbilio lao. 

UTT AMIS - Mshirika hakika katika uwekezaji.

No comments: