Wednesday, August 3, 2016

Usajili Rock City Marathon waanza; RC Mongella awa wa kwanza kujisajili


Mkuu wa mkoa wa Mwanza ndg John Mongella (alievaa kofia nyeusi) sambamba na Rais wa Chama cha Riadha Tanzania ambae pia ni mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka ( wa kwanza kulia) wakisaini fomu za ushiriki wa Rock City Marathon inayotarajiwa kufanyika September 25 mwaka huu katika viwanja vya CCM Kirumba jijini Mwanza. Anaeshuhudia ni Makamu Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi yam bio hizo Bw Zenno Ngowi (wa tatu kulia)
ais wa Chama cha Riadha Tanzania ambae pia ni mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka (kulia) akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo Bw Zenno Ngowi (kushoto) fomu za ushiriki wa Rock City Marathon inayotarajiwa kufanyika September 25 mwaka huu katika viwanja vya CCM Kirumba jijini Mwanza baada ya kusaini ili kuthibitisha ushiriki wake kwenye mbio hizo. Anaeshuhudia (katikati) ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza ndg John Mongella.
Meneja Mkuu wa Mwanza Hotel Bw Senthil Kumar (wa pili kulia)ambaye ni moja wa wadhamini wa mbio hizo akiwa na baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia kwa umakini hotuba ya mgeni rasmi.
Makamu Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo Bw Zenno Ngowi akitoa taarifa fupi kuhusu mbio hizo mbele ya mgeni rasmi na wageni waalikwa.
Rais wa Chama cha Riadha Tanzania ambae pia ni mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka akizungumza kuhusu mbio hizo wakati hafla hiyo.
Mgeni rasmi ambae ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza ndg John Mongella akizungumza kwenye hafla hiyo. Pamoja na mambo mengine Bw Mongella alielezea adhma yake ya kushirikia mbio za kilomita 21 kwenye Rock City Marathon.
Mgeni rasmi ambae ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza ndg John Mongella ( mwenye kofia nyeusi) pamoja na Rais wa Chama cha Riadha Tanzania ambae pia ni mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka (watatu kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na waandaaji wa Rock City Marathon, wadhamini na maofisa wa michezo kutoka mkoa wa Mwanza.



Mkuu wa mkoa wa Mwanza ndg John Mongella jana alikuwa mtu wa kwanza kujisajili kushiriki Rock City Marathon inayotarajiwa kufanyika September 25 mwaka huu katika viwanja vya CCM Kirumba jijini humo.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa mbio hizo mkoani humo Bw Mongella aliekuwa ameambatana na Rais wa Chama cha Riadha Tanzania ambae pia ni mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka, pamoja na viongozi wengine wa mchezo huo alitoa pia aliahidi kukimbia mbio za kilomita 21 ili kuonyesha nia ya dhati katika kuinua mchezo huo uliolipa taifa heshima miaka ya nyuma.

“Nitamke rasmi kwamba kwa sasa Rock City Marathon ni agenda ya mkoa na hivyo basi nitahakikisha kwamba mbio hizi zinapata washikiriki wa kutosha sambamba na wadhamini kutoka mkoa huu. Haiwezekani mbio za mkoa wa Mwanza zitegemee wadhamini wengi kutoka Dar es Salaam huku Mwanza kukiwa na makampuni na mashirika yenye uwezo wa kuusaidia mkoa wao,’’ alisema.

Kwa mujibu wa Bw Mongella msukumo wake huo kwenye ushiriki wa mbio hizo unatokana na si tu nia ya kuinua mchezo huo mkoani mwake bali pia malengo ya mbio hizo ya kutangaza utalii wa ndani wa mkoa huo pamoja na kupinga vita ujangili hususani mauaji ya tembo.

Kwa upande wake Bw Mtaka mbali na kuwapongeza wadhamini wa mbio hizo yakiwemo mashirika ya Freidkin Conservation Fund na African Wildlife Trust pia alitoa wito kwa makampuni mengine ya hifadhi na kitalii yafikirie kutumia fursa hiyo kutangaza utalii wa ndani.

“Pamoja na kuwapongeza waandaaji wa mbio hizi pia yaani kampuni ya Capital Plus International naomba nitoe wito kwao kuhakikisha wanaandaa utaratibu wa kuwaandaa washiriki wa mbio hizo miezi mitatu kabla kwa kuhakikisha wanapata mazoezi ya kutosha ili kama taifa tuwe na matokeo mazuri dhidi ya washiri kutoka mataifa ya nje,’’ alisisitiza.

Akizungumzia mbio hizo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo Bw Zenno Ngowi alisema Mbio hizi zinafanyika kwa mara ya nane mfululizo tangu zianze mwaka 2009 zikiwa na lengo la kusaidia utambuzi, uhamasishaji na uibuaji wa vipaji vya riadha nchini kuanzia umri mdogo kabisa sambamba na kutangaza utalii wa ndani kupitia michezo.

Zaidi Bw Ngowi aliwashukuru wadau mbalimbali wa michezo hapa nchini zikiwemo kampuni za Freidkin Conservation Fund, African Wildlife Trust, Mwanza Hotel, Nyanza Bottlers Limited, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),na kampuni ya ujenzi kutoka China ya CRJE na kampuni ya Real PR Solutions kwa kudhamini mbio hizo.

Kwa upande wake Mratibu wa Mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus Bw Mathew Kasonta alisema Rock City Marathon zitahusisha makundi matano yaani mbio za kilomita 21 kwa wanaume na wanawake, kilomita 5 kwa ngazi ya ‘corporate’, kilomita 3 kwa ajili ya walemavu na zile za wazee umri zaidi miaka 55 na kuendelea pamoja na kilomita 2 kwa ajili ya watoto umri kati ya miaka 7 hadi 19.

Pia litoa wito kwa wakazi wa jiji la Mwanza na mikoa jirani kujisajili kwa kuchukua fomu katika ofisi za michezo kwenye mikoa na wilaya zote za mkoa huo.

“Kwa upande wa Dar es Salaam Fomu za ushiriki pia zinapatikana katika ofisi za Kampuni ya Capital Plus International zilizopo ghorofa ya tatu jengo la ATC, jijini Dar es, Salaam na vituo vingine vitatangazwa hivi karibuni,” alihitimisha.

No comments: