Wednesday, July 27, 2016

WAZIRI SIMBACHAWENE ATEMBELEA RUVUMA NA KUKAGUA MAJENGO YA SHULE.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Raid TAMISEMI George Simbachawene akikagua jengo la darasa la while ya msingi Luegu wilaya ya Namtumbo baada ya kupata maafa mwaka uliopita.Waziri ametoa agizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo kutoa fedha  shilingi milioni 10 kwa ajili ya Ujenzi wa vyoo vya kudumu vya wanafunzi ndani ya mwezi mmoja.
 Wanafunzi wa kidato cha Tano shule ya sekondari Nasuli wilaya ya Namtumbo wakimsikiliza Waziri Simbachawene alipotembelea shule ambayo imeanzisha madarasa ya kidato cha tano mwaka huu.Jumla ya wanafunzi 90 wasichana wameanza masomo hadi  sasa.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt.Binilith Mahenge akimpongeza  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI George Simbachawene alipomaliza kukagua ujenzi wa barabara  ya lami ya FFU-Matogoro yenye urefu wa kilometa 3.2 kwenye Manispaa ya Songea.
 Jengo la makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea lililokamilika kujengwa ambalo leo  limekaguliwa na Waziri Simbachawene kwenye kijiji cha Lundusi,Peramiho.Waziri Simbachawene ameagiza ifikiapo tarehe 05 Agosti 2016 watumishi wote wa Halmashauri ya wilaya ya Songea wahamie na kuendelea na kazi baada ya kukamilika ujenzi wake.
Wananchi wa kijiji cha Lundusi Peramiho wakiwa kwenye mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri wa Nchi Ofisi  ya Rais  TAMISEMI George Simbachawene(hayupo pichani) wakati wa ziara yake  Mkoani Ruvuma leo

No comments: