Thursday, July 14, 2016

WAZIRI MBARAWA ATEMBELEA VIWANJA VYA NDEGE JULIUS NYERERE

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Maafisa Uhamiaji katika Kiwanja cha Ndege Cha Kimataifa Cha Julius Nyerere(Terminal II), alipotembelea kuangalia utendaji kazi na vifaa vya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akitoa malekezo wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi George Sambali (Katikati), alipotembelea Mamlaka hiyo.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akitoa malekezo wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi George Sambali (Katikati), alipotembelea Mamlaka hiyo.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akitoa malekezo wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi George Sambali (Katikati), alipotembelea Mamlaka hiyo.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akizungumza na Mawakala wanaofanya kazi  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA),alipotembelea kuona utendaji kazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA). 
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Swissport, Gaudence Temu, wakati alipotembelea Ofisi hiyo jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) hawapo pichani, wakati alipoongea nao jijini Dar es Salaam. 
                                                   (Picha na Benjamin Sawe- Maelezo)
WAZIRI MBARAWA AIAGIZA TAA KUONGEZA MAPATO.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ameiagiza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuongeza kiwango cha ukusanyaji mapato kutoka Bilioni 74 hadi kufikia bilioni 105 katika mwaka wa fedha 2016/2017.

Ametoa agizo hilo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka hiyo mara baada ya kukagua majengo matatu na ofisi mbalimbali zilizopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNIA).
Amesisistiza wafanyakazi wa Uwanja huo kuhakikisha kiasi cha ukusanyaji wa mapato hayo kinaongezeka siku hadi siku ili kukuza uchumi wa taifa na kuchochea fursa za kimaendeleo.

“Ni lazima muongeze kasi ya kufanya kazi ili mapato yaongezeke kwa kuwa uwezo mnao na nimeona kwenye viwanja vyenu kuna sehemu nyingi za biashara, hivyo mna kila sababu ya kukusanya kiasi hicho cha fedha”, amesema Prof. Mbarawa.

Aidha, katika ziara hiyo Waziri Prof. Mbarawa alibaini ucheleweshwaji wa vibali kwa abiria wanaoingia katika Uwanja wa Ndege wa  JNIA ambapo abiria huchukua zaidi ya saa moja kupata vibali.

“Nimesikitishwa na kitendo cha ucheleweshwaji wa vibali kutoka Idara ya Uhamiaji na huduma za kibenki zinazotolewa… hali hii haileti picha nzuri kwa wageni wetu. Abiria kuwekwa zaidi ya saa moja akisubiri kupata huduma, sitaki kuona hali hiyo ikiendelea”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Sambamba na hilo amezitaka taasisi zote zinazofanya kazi katika viwanja vya ndege kushirikiana kwa ukaribu ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma na kuongeza mapato kwa taifa.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Eng. George Sambali amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa mapungufu yaliyobainishwa yatafanyiwa kazi ili kuongeza ufanisi na huduma bora kwa abiria.
“Kwa kushirikiana na taasisi zote ambazo zinafanya kazi katika Kiwanja hiki tutahakikisha tunatoa huduma nzuri na kuongeza ufanisi katika utendaji ili kufikia malengo”, amesema Eng. Sambali.

Waziri Prof. Mbarawa amefanya ziara ya siku moja katika Kiwanja cha JNIA ili kuona utendaji kazi na maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Tatu la abiria ambapo jengo hilo linatarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2017 na litakuwa na uwezo wa kuhudumia zaidi ya abiria milioni sita kwa mwaka.


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano .

No comments: