Saturday, July 16, 2016

WANAFUNZI WENYE WAZO NZURI LA BIASHARA KUWEZESHWA NA VIONGOZI WA CHUO CHA ACHARYA.

VIONGOZI wa Chuo cha Acharya cha Nchini India wawakutanisha watanzania waliosoma katika chuo Acharya jijini Dar es Salaam leo.


Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Mwenyekiti wa Chuo Acharya huko nchini India, Premnath Reddy amesema kuwa wapo tayari kuwasaidia wanafunzi waliosoma katika chuo cha Acharya watakaoanzisha wazo zuri la biashara.
"Tupo tayari kusaidia wanafunzi watakao kuwa na wazo zuri la kibiashara kwa wanafunzi waliosoma nchini India katika chuo cha Acharya " Amesema Reddy.

Hayo amesema kwa wanafunzi hao ili kutokuteemea kuajiliwa tuu na waweze kujiajili wenyewe kutokana na elimu waliyoipata wakiwa chuoni.
Mwananfunzi aliyesoma kuchu cha Acharya nchini India, Sakina Naushad Karmali akizunguma jijini Dar es Salaam na wanafunzi waliosoma katika chuo cha Acharya

Mkurugenzi wa chuo cha Acharya cha nchini India, Vishesh Chanrashelear akizungumza na wanafunzi wa kitanzania waliosoma katika chuo cha Acharya katika hafla iliyowakusanya jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chuo Acharya huko nchini India, Premnath Reddy akizungumza na wanafunzi wa hapa nchini waliosoma chuo cha Acharya kwanzia mwaka 2009 hadi mwaka huu katika hafla fupi iliyowakutanisha jijini Dar es Salaam na kula na kunywa pamoja.
 Watanzania waliosoma India chuo cha Acharya wakiwa wamesimama na kuimba wimbo wa Taifa wakati wa hafla iliyowakutanisha wanafunzi waliosoma chuo kimoja.
 Muunguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Mwanafunzi aliyewahi kusoma katika chuo cha Acharya, Christina Mwandalima akizungumza na wanafunzi wenzie pamoja na viongozi wa Chuo chao  waliofika kujumuika pamoja na kula na kunywa pamoja.

Mwanafunzi wa chuo cha Acharya akizungumza katika mjumuiko wa wanafunzi wa chuo chao jijini Dar es Salaam.

No comments: