Thursday, July 14, 2016

SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LATUNUKIWA TUZO TATU KWA UBORA WA HUDUMA ZA ANGA

Makamu wa Rais wa Huduma wa Shirika la Ndege la Etihad, Sajida Ismail, Makamu wa Rais wa Uhusiano wa shirika hilo, Calum Laming akipokea tuzo za Skytrax World Airline ya World Best First Class Airline, World’s Best First Class Onboard Catering na World’s Best First Class Airline Seat

Shirika la ndege la Etihad limetunukiwa tuzo tatu za ubora wa juu kwenye madaraja  pia tuzo ya ubora kwenye huduma za vyakula pia  tuzo ya ubora kwenye malazi  kutoka Skytrax Worldairline Awards, zilizotangazwa NCHINI uingereza.

Tuzo hizo za World Airline ni za kimataifa na huhusisha mashirika ya ndege yanayofanya vizuri katika sekta ya usafiri wa anga. Mshindi huchaguliwa kwa kura kutokana na mchakato ambao huchukua miezi 10 kukamilika kwake huku ikujumuisha wasafiri takribani milioni 18 kutoka katika nchi zaidi ya 100 ulimwenguni.

Makamu wa Rais wa Shirika la Etihad kwenye masuala ya wageni alisema,“ Mwaka 2014 tuliingia kwenye ushindani kwa kutambulisha ndege yetu ya abiria Airbus A380 na Boing 787 Dreamliner. Jambo hili limeonyesha dhamira yetu ya kuwa wa kwanza katika kutoa huduma ya kisasa na uvumbuzi.”

“Ninafarijika na jambo hili ikiwa ni matokeao ya uwekezaji wa huduma bora kwa wateja wetu ulimwenguni, kwa mara nyingine tena tumetunukiwa tuzo hizo za kuwa wa kwanza kwa ubora katika huduma za kuwa na madaraja yenye hadhi.  Tuzo hii itakuwa chachu katika kuongeza nguvu kwenye kuwekeza zaidi kwenye bidhaa zetu na huduma za usafiri.”

Katika miaka ya hivi karibuni, shirika laetu limepata tuzo ya kuwa wa kwanza kwenye huduma zetu. Hii ni mara ya pili kwa kupata tuzo na kipekee kupata tuzo tatu kwa pamoja ikiwa ni shirika pekee kunyakua tuzo hizo.

Mwnyekiti wa Skytrax, Edward Plaisted alisema “Shirika la Ndege la Etihad limekuwa likiimarika na kuwa bora zaidi katika usafiri wa anga kwa kuendana na mabadiliko ya teknolojia ya kisasa katika utoaji wa huduma zake na ukarimu. Kwa mara nyingine tena shirika hili limenyakua tuzo tatu muhimu kwa kupigiwa kura na amamilioni ya wasafiri ulimwenguni kote, ambapo ni dhahili ilistahili kuwa mshindi kutokana na kutoa huduma za kiwango cha juu.”
Kuwapo kwa huduma nzuri za maradhi kwa wasafiri, vyumba nanae vya kulala vya hadhi ya juu, eneo zuri na la kipekee kwa abria kupumzika likiwa na ukubwa wa kutosha ni mambo yaliyopelekea kupata tuzo ya ubora.

Kuwapo kwa ndege ya 787 ambayo ina ambayo imesheheni vitu mbalimbali ndani yake ikiwamo vyumba vyenye vitanda, runinga kubwa ya kisasa, eneo la kulia chakula na madhari ya kuvutia ni miongoni mwa mambo yaliyoipa tuzo ya kuwa wa kwanza kwenye ubora wa hali ya juu.

Shirika la Ndege la Etihad kwa kutumia ndege zake za Boeing 777 ana Airbus A330/A340 itaendelea kutoa huduma bora kwa wateja zikiwa na viti vyenye mwonekano na mazingira mzuri kwa mtumiaji.

Ndege za shirika la Etihad zimekuwa zikitoa huduma bora zaidi za hoteli ndani ya ndege zake ili kukidhi mahitaji ya wateja wake. Katika hoteli zake ndani ya ndege kuna huduma ya vyakula vya aina mbalimbali ambavyo vinaandaliwa na watu wenye uzoefu. Na huduma ya chakula inatolewa kwa madaraja yote kwenye ndege za Etihad. Pia wateja wana fursa ya kujadiliana na watoa huduma kwenye ndege kulingana na mahitaji yao ya chakula.

Wageni wanaweza kuchagua chakula wanachokipenda kwenye menu zinazopatikana kwenye hoteli za kwenye ndege.
Aidha katika Uwanja wa Kimataifa wa Abu Dhabi kumefunguliwa mgahawa ambao utahudumia wateja wa Etihad ukiwa na vitu mbalimbali muhimu ambavyo vitakidhi mahitaji ya mteja ikiwa na lengo kila mteja apate huduma bora inayomfaa.

No comments: