Tuesday, July 19, 2016

SERIKALI INAPOTEZA SH.BILIONI 18 KUTOKANA NA KUKOSA RADA.

SERIKALI inapoteza shilingi bilioni 18 kutokana na kukosa rada za kuongezea ndege na kufanya nchi ya Kenya ipate mapato hayo kwa kuwa rada.

Hayo ameyasema leo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani wakati wa Mkutano wa kwanza wa Wamiliki wa Ndege wa Afrika Mashariki na Afrika (IATA), amesema kuwa kutokana na Serikali kukosa mapato wameagiza rada mbili ambazo zitagharimu dola za Kimarekani Milioni 24.

Ngonyani amesema kuwa 
rada hizo mbili zitafungwa nusu ya anga la Tanzania ambazo
 zitafanya serikali ya Tanzania kupata fedha kutokana na ndege zitazotumia mawasiliano ya Rada kulipia ambapo kwa sasa hatuna uwezo huo.

Amesema kuwa katika mkutano huo shirika la ndege Presion ndio mwanachama wa IATA huku Shirika la Ndege za Serikali (ATCL) likikosa sifa kuwa mwanachama kutokana ndege zake kushindwa kukidhia vigezo vilivyowekwa.

Ngonyani amesema kuwa kutokana na mkakati wa serikali kwa sasa wanatarajia kununua ndege mbili za kisasa na baadae kuongeza ndege zingine katika kutoa huduma ya wananchi na kwenda hadi nje ya Afrika.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga, Hamza Johari amesema kuwa wanaendelea katika kuboresha huduma za anga.
Imeandaliwa na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akizungumza katika mkutano wa kwanza wa wamiliki wa ndege wa Afrika mashariki na na Afrika kwa ujumla (IATA) jijini Dar es Salaam. Pia katika mkutano huo wanaanalia changamoto mbalimbi katika sekta ya usafiri wa Anga.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga, Hamza Johari akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa
 kwanza wa Wamiliki wa Ndege wa Afrika Mashariki na Afrika (IATA) uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wa wadau na wamiliki wa ndege wakiwa katika 
Mkutano wa kwanza wa Wamiliki wa Ndege wa Afrika Mashariki na Afrika (IATA) ulioanyika leo jijini Dar es Salaam.

No comments: