Thursday, July 7, 2016

MWENYEKITI WA BODI YA NSSF, MSAJILI WA HAZINA NA KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI, MAWASILINO NA UCHUKUZI WATEMBELEA BANDA LA NSSF

 Meneja kiongozi wa Masoko na Uhusiano Eunice Chiume akimpatia Maelezo juu ya Mradi wa Nyumba wa Kijichi Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF Prof. Samwel Wangwe alipotembelea Banda la NSSF kwenye Maonesho ya 40 ya biashara ya Kimataifa.
 Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Joseph Nyamhanga akifurahia baada ya kupewa maelezo juu ya Miradi ya Nyumba ya Mtoni Kijichi, Toangoma na Dungu Farm, Miradi hiyo iliyopo kigamboni imevutia watu wengi kutokana na urahisi wake wa kufikika kupitia Daraja la Nyerere.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Joseph Nyamhanga akifurahi baada ya kupewa Maelezo ya Mradi wa Viwanja Vya Kiluvya na Meneja kiongozi Masoko na Uhusiano wa NSSF Eunice Chiume alipotembelea banda la NSSF.
Msajili wa Hazina Lawrence Mafuru akifurahia maelekezo aliyokuwa akipewa na Meneje Kiongozi wa Masoko na Uhusiano Eunice Chiume alipotembelea banda la NSSF kwenye maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara.
Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru akipewa maelezo katika idara ya wakala wa bima wa NSSF na Afisa Bima Isack Peter alipotembelea banda la NSSF, akishuhudia katikati ni Meneja kiongozi Masoko na Uhusiano Eunice Chiume.
Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume akimuelezea Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF Prof. Samwel Wangwe Jinsi ya kutoa mrejesho wa Huduma za NSSF alipotembelea banda la NSSF.

No comments: