Tuesday, July 5, 2016

MRADI WA USAID WA UIMARISHAJI MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA (PS3) WAZINDULIWA MKOANI KIGOMA


 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali (Rt), Emmanuel Maganga akizindua mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) katika mkoa wake wa Kigoma leo. Mradi huo wa miaka mitano unafadhiliwa na Shirika la Misaada la Kimataifa la Marekani (USAID)  na utatekelezwa katika mikoa 13 nchini na kushirikisha Halamashauri 93.
 Mkuu wa Mkoa aliwataka watendaji wa Halamashauri hizo kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha mradi unaleta manufaa kwa jamii na mkoa.
 Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Charles Pallangyo, akizungumza wakati wa uzinduzi huo. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mjini   Samsoni Anga, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali (Rt), Emmanuel Maganga, Kiongozi wa Mradi wa PS3, Dk Conrad Mbuya na Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi.
Kiongozi wa mradi wa PS3, Dk Conrad Mbuya akizungumza na kueleza dhumuni la mradi huo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Brigedia Jenerali (Rt), Emmanuel Maganga.
 Mwakilishi kutoka Tamisemi, Mrisho Mrisho akizungumza kuhusiana na mradi huo na namna ambavyo serikali imejipanga kuhakikisha utekelezaji wake unafanikiwa.
Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Kigoma wakifuatilia kwa makini uzinduzi huo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya  Buhigwe, Kanali. Elisha Marco Gaguti, Mkuu wa Wilaya ya  Kakonko    Kanali.Hosea Malonda Ndagala na Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Luis Peter Bura.
 Mkuu wa Wilaya Kasulu,  Kanali. Martin Elia Mkisi akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwanamvua Hoza Mlindoko, wakifuatilia mada katika uzinduzi huo. 
 Msimamizi wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) Dk Conrad Mbuya akiwasilisha mada baada ya kufanyika kwa uzinduzi.

UZINDUZI wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), umefanyika mjini Kigoma siku ya Jumatatu na Jumanne, Julai 4-5, 2016. Mradi huo ujulikanao kwa Kiingereza kama Public Sector Systems Strengthening (PS3) ni wa miaka mitano, na utafanya kazi na Serikali Kuu pamoja na Halmashauri 93 katika mikoa 13 ya Tanzania bara.

PS3 inalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa taarifa, na tafiti tendaji. Ushirkiano huu wa PS3 katika ngazi ya Serikali kuu na Halmashauri, una nia ya kukuza utoaji, ubora, na matumizi ya huduma za umma, hususan kwa jamii ambazo hazijanufaika vya kutosha katika uzinduzi huo, mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa waKigoma, Mh. Brigedia Jenerali (Mstaafu) Emmanuel Maganga. Watu takribani 250 walihudhuria.

Washiriki wa uzinduzi huo walikuwa ni: Katibu Tawala wa Mkoa (RAS), Wakuu wa Wilaya za Lindi, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa, na Wajumbe wa Timu ya Mejenimenti kutoka kwenye Halmashauri. Mkoa wa Kigoma una Halmashauri nane, ambazo ni: Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma, Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko, Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, na Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe.

PS3 ni mradi wa miaka mitano ambao umeandaliwa na USAID kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, na unafadhiliwa na USAID. Unatekelezwa na mashirika saba yakiwepo ya kitaifa na kimataifa, ambayo ni: Abt Associates Inc., kama mtekelezaji mkuu, na watekelezaji wasaidizi ambao ni Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Mafunzi ya Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI), Taasisi ya Ushauri Tanzania (TMA), Broad Branch Institute, Intra Health International, na Urban Institute. Mikoa 13 ya Tanzania Bara ambako mradi utatekelezwa ni: Iringa, Dodoma, Kagera, Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, na Shinyanga.


MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA
PS3 itaimarisha mifumo katika ngazi ya Taifa, Mkoa na Halmashauri. Mradi utahakikisha mifumo iliyopo katika ngazi ya Halmashauri inaimarishwa kupitia kitita cha afua zilizoundwa kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi wa Tanzania. Mafanikio yanayotarajiwa ni pamoja na:

Utawala Bora na Ushirikishwaji wa Raia: Uimarishaji wa utawala katika ngazi ya kitaifa na ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, ili kuweza kutumia rasilimali kwa uwazi, kuwezesha ushiriki wa wananchi katika kupanga, kufuatilia, na kutoa matokeo katika kila sekta.

Rasilimali Watu: Kuongezeka kwa usawa katika mgawanyo wa rasilimali watu kwa ajili ya utoaji wa huduma bora kwenye maeneo yenye uhitaji zaidi. Kuimarisha mfumo wa ajira pamoja na kudumu kwa watumishi katika ajira serikalini.

Fedha: Ongezeko la pato la ndani kwa ajili ya huduma za umma, kuongeza ufanisi katika matumizi ya fedha za umma, na pia kuongeza uwiano kati ya kiasi cha fedha kilichotumika na mali iliyonunuliwa.

Mifumo ya Mawasiliano: Kuimarisha mifumo ya utoaji taarifa iliyopo nchini, pamoja na matumizi ya takwimu kwa wadau.

Utafiti Tendaji: Tafiti Tendaji muhimu zitakazosaidia mradi kujua changamoto na mikakati ya kuzishughulikia changamoto hizo. Tafiti hizi zitasaidia kugundua fursa zilizopo na kuzitumia kuweza kupata matokeo yanayotarajiwa. Pia tafiti hizo zitasaidia kuboresha maamuzi serikalini.
 Dk Gemin Mtei akiwasilisha mada kuhusiana na mikakati ya kufanikisha mradi huo.
 Aloyce Maziku kutoka PS3 akiwasilisha mada kuhusiana na Tafiti Tendaji.
 Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Mwanamvua Mlindoko akifuatilia mada hizo kwa makini.
Washiriki wakifuatilia mada kwa umakini.
 Mkuu wa Wilaya ya  Buhigwe, Kanali. Elisha Marco Gaguti akisikiliza kwa makini.
 Mkuu wa Wilaya ya  Kakonko    Kanali.Hosea Malonda Ndagala akiwa makini kusikiliza mada zinazowasilishwa.
 Wakuu wa Wilaya na washiriki wengine wakifuatilia mada.
 Benchi la Ufundi la mradi wa PS3 wakiwa kazini.
 Washiriki wakiuliza maswali
 Matiko Machonchoryo akijibu moja ya maswali yaliyoulizwa.
 Mshauri wa Habari na Mawasiliano katika Mradi wa PS3, Leah Mwainyekule akielezea jambo.
 washiriki wakiwa mkutanoni.
 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma (wapili kulia) akiagana na Msimamizi wa mradi wa PS3, Dk Conrad Mbuya baada ya uzinduzi. Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma mjini,Samsoni Anga.
 Picha za pamoja na makundi mbalimbali.
Picha ya pamoja kati ya viongozi na waratibu wa mradi wa PS3.

No comments: