Saturday, July 30, 2016

MASAUNI AONGOZA MSAFARA WA MABALOZI WA USALAMA BARABARANI KUJIFUNZA KAZI ZA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI, JIJINI DAR

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Mabalozi wa Usalama Barabarani pamoja na Askari na Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mara baada ya Naibu Waziri huyo na Mabalozi hao kuonyeshwa shughuli mbalimbali zinazofanywa na Jeshi hilo. Katika hotuba yake Masauni aliwataka Mabalozi hao waendelee kushirikiana na Wizara yake katika kupambana na ajali nchini. Tukio hilo lilifanyika katika Kituo cha Zimamoto, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto (meza kuu), Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Thobias AndengenyeNaibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia) akipokea maelezo kutoka kwa Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ni Kamanda wa Jeshi hilo Mkoa wa Ilala, Ully Mbuluko jinsi chumba cha mawasiliano kinavyopokea miito mbalimbali ya matukio ya majanga. Masauni aliongoza msafara wa Mabalozi wa Usalama Barabarani ambao walifanya ziara ya kujifunza kazi za Jeshi hilo katika Kituo cha Zimamoto, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiangalia Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakizima moto wakati tukio la moto linapotokea. Masauni aliongoza msafara wa Mabalozi wa Usalama Barabarani ambao walifanya ziara ya kujifunza kazi za Jeshi hilo katika Kituo cha Zimamoto, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam.Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwa amevaa mtungi wa hewa safi na salama ambao utumiwa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pindi anapokosa hewa wakati wa tukio la uzimaji moto au maokozi. Kushoto ni Mrekebishaji wa Vifaa vya Kupumulia wa Jeshi hilo, Sajini Paul Mwenda. Wapili kushoto ni Mkuu wa Jeshi hilo, Kamishna Jenerali Thobias Andengenye. Masauni aliongoza msafara wa Mabalozi wa Usalama Barabarani ambao walifanya ziara ya kujifunza kazi za Jeshi hilo katika Kituo cha Zimamoto, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiwaangalia Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakionyesha jinsi wanavyofanya uokoaji wakati ajali mbalimbali zinapotokea nchini. Masauni aliongoza msafara wa Mabalozi wa Usalama Barabarani ambao walifanya ziara ya kujifunza kazi za Jeshi hilo katika Kituo cha Zimamoto, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto) akimsikiliza Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye (kushoto) alipokuwa anatoa maelezo jinsi Jeshi lake linavyofanyakazi katika matukio mbalimbali ya uzimaji moto au uokozi yanapotokea nchini. Masauni aliongoza msafara wa Mabalozi wa Usalama Barabarani ambao walifanya ziara ya kujifunza kazi za Jeshi hilo katika Kituo cha Zimamoto, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam.(PICHA ZOTE NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI).

No comments: