Monday, July 4, 2016

KAMPUNI YA AFRI TEA AND COFFEE BLENDERS 1963 LTD YAIBUKA KIDEDEA MAONESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA, WANYAKUA TUZO YA MSHINDI WA KWANZA ‘MAONESHO BORA YA BIDHAA ZA VYAKULA VINYWAJI’ 2016.


 Rais wa Rwanda Paul Kagame, (wa pili kulia) akimkabidhi Mkuu wa Idara ya Masoko, Biashara ya Nje na Wateja, Bw. Zachy Irenus Mbena, Tuzo ya Mshindi wa Kwanza wa Maonesho ya Bidhaa Bora za Vyakula na Vinywaji 2016, wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jana Julai 2.
******************************
Na Ripota wa Sufianimafoto, Dar
KAMPUNI ya Kitanzania ya Afri Tea and Blrenders (1963) Ltd, inayozalisha bidhaa bora zinazotangaza vivutio mbalimbali na Uchumi wa Tanzania kama Majani ya Chai ya Green Label, African Pride Tea, Kilimanjaro Infusions, Simba Chai, Kahawa ya Africafe na Uji Bora, wameibuka kidedea katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa kwa kunyakua Tuzo ya Mshindi wa Kwanza wa Maonesho ya Bidhaa Bora za Vyakula na Vinywaji 2016.
Akizungumza na Mtandao huu Mkuu wa Idara ya Masoko, Biashara ya Nje na Wateja, Bw. Zachy Irenus Mbena, alisema kuwa hii ni Tuzo ya tatu kwa mwaka wa tatu mfululizo kupata ambapo mwaka 2014 wapitwaa Tuzo ya mshindi wa kwanza, 2015 walipata Tuzo ya mshindi wa pili ya Wauzaji wa Bidhaa za Tanzania Nje ya Nchi (Best Exporting) na mwaka  huu wamerejea katika nafasi ya kwanza.
Aidha Mbena alisema kuwa anawashukuru waeteja na watumiaji wa bidhaa zao waliowafanya kuweza kutambulika Kimataifa kwa kutangaza Uchumi, Vivutio na Utalii wa Tanzania kupitia bidhaa zao kama Mlima Kilimanjaro, Wanyama, Khanga Vazi la asili ya Kimasai na Utamaduni wa Mtanzania kwa ujumla.
Kampuni hiyo imezidi kujizolea sifaa kabambe kwa kuwa wabunifu katika kuzalisha Bidhaa zinazoendana na mahitaji halisi ya Watanzania.
Aidha Kampuni hiyo imezalisha bidhaa pekee inayotangaza Kisiwa cha Zanzibar ‘Africafe Zanzibar Spice Coffee’ iliyochanganywa na Karafuu huku ikiwa katika muonekano wa kuvutia inajitangaza kimataifa, iliyohifadhiwa katika Kasha lililonakshiwa ramani ya Kisiwa cha Zanzibar na baadhi ya alama za Kisiwa hicho.
‘’Pamoja na hayo lakini pia tunashiriki katika maonesho mbalimbali ya Nje ya nchi yanayoandaliwa na Mabalozi wetu wa Tanzania nchi za Nje ‘Tanzania Day in Embasses’ ambapo mwezi uliopita tulialikwa kushiriki  maonesho yaliyofanyika katika jiji la Antalya Uturuki, ambayo pia yalishafanyika Msumbiji, Uingereza, Ethiopia na Rusia’’. Alisema Mbena
Pia wamekuwa wakushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Maendeleo ya Biashara Tanzania ‘TAN TRADE’ katika maonesho mbalimbali ya Kimataifa.
Kutokana na umuhimu na ubora wa bidhaa zao zinazotengenezwa kiasili, wamekuwa wakishiriki pia katika maonesho mbalimbali ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane katika Mikoa ya Mbeya, Arusha na Morogoro.
Aidha Bw. Mbene aliwakaribisha Wanzania wote wanaofika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere kutembelea Mabanda ya maonesho kufika katika Banda lao linalotoa huduma kufuturisha BURE kwa wafungaji mida ya jioni ambao hupewa fursa ya kuonja chai za aina zote pamoja na Chai, Uji ,Kahawa na Maji bila malipo yeyote.
Pamoja na hayo pia wananchi wanaofika katika Banda hilo hupewa zawadi ya Pakiti moja Majani ya Chai yenye mchanganyiko wa radha tofauti tofauti za Green Tea,  Hibiscus, Rooibos, Paper Minty, Camomile, Vanilla na Morocco Minty.
 Muonekano wa Banda la Maonesho la Afri Tea and Blrenders (1963) Ltd.
 Afisa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Afri Tea and Coffee (1963) Ltd, Sheila Manafi, akipozi na Tuzo waliyokabidhiwa na Rais Kagame.
Baadhi ya Wananchi waliofika katika Banda hilo wakinunua na kuonja radha tofauti za Chai za Kampuni hiyo.
 Muonekano wa Mandhari ya banda hilo lililo katika maonesho hayo likiwa na baadhi ya vitu vyenye muonekano wa Tamaduni za Kitanzania.
 Baadhi ya Wananchi waliofika katika Banda hilo wakionja radha za Chai na Kahawa za Kampuni hiyo.
 Mfanyakazi wa Kampuni hiyo, Cecilia Mrema (kulia) akitoa maelezo kwa baadhi ya wateja katika Banda hilo.
 Mfanyakazi wa Kampuni hiyo, Ronne Zachy (kushoto) akifafanua jambo kwa baadhi ya wateja waliotembelea Banda hilo.
 Sheila akipanga bidhaa.....
 Baadhi ya wateja wakipata maelezo kutoka kwa wahudumu wa Kampuni hiyo
  Mfanyakazi wa Kampuni hiyo, Cecilia Mrema (kulia) akitoa maelezo kwa baadhi ya wateja katika Banda hilo.
 Baadhi ya wananchi waliofika katika Banda hilo wakionja radha tofauti za Chai na Kahawa za Kampuni hiyo.
 KARIBU KATIKA BANDA LA MAONESHO LA KAMPUNI YA AFRI TEA AND COFFEE BLENDERS 1963 LTD KATIKA MAONESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA SABASABA 2016.

No comments: