Monday, July 4, 2016

KADI ZA VISA ZA BancABC KUPUNGUZA WIZI WA PESA






Mkuu wa Kitengo Cha wateja binafsi na wafanya baishara wadogo wa BancABC, Bi Joyce Malai akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kadi ya VISA ya BancABC maalum kwa wateja wao na hata wasio wateja wao. BancABC imezindua kadi hiyo ya Visa ili kupunguzia wateja adha kubwa ya kubeba fedha tasilimu wanaposafiri ndani na nje ya nchi. hafla ya uzinduzi ilifanyika jana viwanja vya sabasaba
Mkuu wa Masoko wa BancABC, Bi Upendo Nkini, akielezea faida za kadi Mpya ya VISA ya BancABC inayomwezesha mteja kufanya malipo ya mtandaoni kwa urahisi kwa kuwa kadi hiyo inalindwa kwa kutumia teknolojia mpya ya CHIP na PIN.
Wafanyakazi wa BancABC kitengo cha huduma kwa wateja Bw, Ally Miraji kushoto na Bi Neema David wakimuhudumia mmoja wa wateja aliyekuwa akichukua kadi ya VISA ya BancABC bw, Fredrick Israel katika banda la Bank hiyo viwanja vya sabasaba. BancABC imezindua kadi hiyo ya Visa ili kupunguzia wateja adha kubwa ya kubeba fedha tasilimu wanaposafiri ndani na nje ya nchi na kwamba ni njia bora ya kufanya malipo kupitia mitandao kwa kuwa imeunganishwa na mitandao ya simu kama Airtel Money, TigoPesa, na Mpesa. mteja ili kupata kadi hiyo sio lazima awe na akaunti ya BacABC. hafla ya uzinduzi ilifanyika jana viwanja vya sabasaba
Wafanyakazi wa BancABC kitengo cha huduma kwa wateja Bw, Ally Miraji kushoto na wenzake wakitoa huduma ya maelekezo kwa bw, Ahmad Ibrahim kuhusu matumizi ya kadi mpya ya VISA ya BancABC katika viwanja vya sabasaba. BancABC imezindua kadi hiyo ya Visa ili kupunguzia wateja adha kubwa ya kubeba fedha tasilimu wanaposafiri ndani na nje ya nchi na kwamba ni njia bora ya kufanya malipo kupitia mitandao kwa kuwa kadi hiyo imeunganishwa na mitandao ya simu kama Airtel Money, TigoPesa, na Mpesa hafla ya uzinduzi ilifanyika jana viwanja vya sabasaba


Kadi ya VISA ya BancABC ndio kadi pekee inayohudumia wateja wa huduma za fedha za mitandao ya simu.

BancABC, ambayo ni sehemu ya Atlas Mara, imekuja na tiba ya kukithiri kwa wizi wa pesa ambao husababishwa na baadhi ya watu kuzunguka na fedha nyingi mifukoni mwao kwani imeanzisha kadi mpya ya Visa ambayo itaweza kujazwa pesa kwa kutumia shilingi ya Tanzania, Rand ya Afrika Kusini, Dola ya Kimarekani, Euro na Pauni ya Uingereza.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo Cha wateja binafsi na wafanya baishara wadogo, Bi Joyce Malai alisema kadi hiyo itaweza kutumiwa na wateja walio na wasio na akaunti za BancABC na kwamba itawapunguzia adha kubwa ya kubeba fedha tasilimu wanaposafiri nadani na nje ya nchi na kwamba ni njia bora ya kufanya malipo kupitia mitandao.

Alisema watatumia maonesho ya Saba Saba kuitangaza kadi hiyo na wateja wataweza kupata kadi ndani ya muda mfupi baada ya zoezi fupi la usajili ambalo ni papo kwa papo. “Ukiwa na kadi hii utaepuka usumbufu mkubwa mno kwani huhitaji kubeba fedha tasilimu na pia sio lazima uwe na akaunti ya benki,” alisema.

Alisema watumiaji wataweza kupata huduma masaa 24, siku saba kwa wiki mahali popote kupitia ATM zaidi ya 400 zenye huduma ya Visa nchini Tanzania ambapo ATM za aina hii zinafikia milioni 1.3 duniani na pia watumiaji wanaweza kufanya miamala kwa watoa huduma zaidi ya 1000 Tanzania na zaidi ya milioni 35 duniani kote.

“Tumepata ushuhuda na mrejesho mzuri kutoka kwa wateja wetu ambao wana watoto wanaosoma nje ya nchi kwani wanaweza kuwatumia fedha za kujikimu kila mwezi bila kuingia gharama za ziada,” alisema.

“Kinachofaya kadi hii ya Visa iwe ya kipekee ni pale ambapo mteja anaweza kuweka fedha kwenye kadi kwa kutumia huduma ya kutuma pesa kupitia simu ya mkononi yoyote na tunajivunia kuwa benki yetu ndio yenye huduma hii pekee kwa sasa,” alisema.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Masoko, Bi Upendo Nkini, faida nyingine za kadi hiyo ni kama vile kufanya malipo ya mtandaoni kwa urahisi zaidi, kuthibiti matumizi kwani utatumia kiasi cha fedha kilichoko kwenye kadi pekee na pia kuwa na amani kwani pesa zinakuwa salama kwani kadi inalindwa kwa kutumia teknolojia mpya ya CHIP na PIN.

Alisisitiza kuwa hii ndio kadi pekee ya Visa Tanzania ambayo unaweza kutumia kwa ruzuku tano ambazoni shilingi ya Tanzania, Rand ya Afrika Kusini, Dola ya Kimarekani, Euro na Pauni ya Uingereza na kwamba kadi hiyo, ambayo inaweza kutolewa kwa mtu kama zawadi, inaweza kutolewa nyingine pindi inapoibiwa au kupotea.

“Kadi hizi zitapatikana katika banda letu lililoko katika maonyesho ya Saba Saba Ukumbi wa Kimataifa lakini pia unaweza kutuma ujumbe mfupi wenye neno VISA ikifuatiwa na Wilaya uliyopo , kwenda namba 15774,” alisema.

Atlas Mara iliinunua BancABC in Juni 2014 huku ikizidi kujitanua Tanzania, , Botswana, Mozambique, Zambia na Msumbiji. Baada ya hapo ilinunua benki mbili nchini Rwanda (BR Commercial na BPR ambazo zinaendelea kukamilisha mchakato wa kuungana).

No comments: