Sunday, June 26, 2016

WATUMISHI eGA WAASWA KUBORESHA MIFUMO YA TEHAMA KUONGEZA UKUSANYAJI WA MAPATO NDANI SERIKALI.

Na Eleuteri Mangi-MAELEZO.

Watumishi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) wameaswa kuweka vipaumbele na mikakati ya kusimamia mifumo ya TEHAMA inayoboresha utendaji kazi na kutoa huduma ili kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ndani ya Serikali.Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki wakati akizindua baraza la wafanyakazi la Wakala hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.

“Nataka mbuni na kutengeneza mifumo tumizi mipya pamoja na kuiboresha mifumo tumizi iliyopo ili kuongeza tija kwenye sekta za kimkakati hususan sekta za afya, kilimo, utalii, elimu, viwanda na biashara” alisema Kairuki.Waziri Kairuki aliyataja maeneo mengine ambayo yanapaswa kuboreshwa katika ukusanyaji na kutiliwa mkazo katika ukusanyaji wa mapato kuwa ni pamoja na sekta za fedha, rasilimaliwatu, ardhi na utambulisho wa taifa.

Hatua hiyo ya eGA ya kuboresha mifumo ya TEHAMA itasaidia Serikali kuimarisha uwezo wake wa kuwa na taarifa juu ya mifumo yake na kukidhi mapato yake na amewataka watumishi hao wazidishe kasi ya utendaji kazi ili kuendana na kauli mbiu ya Serikali ya Awamu ya Tano ya “Hapa Kazi Tu”.

Aidha, watumishi hao wamesisitizwa kuwa kuundwa kwa baraza hilo la wafanyakazi ni moja ya nyenzo ya kuishauri Serikali katika ngazi ya taasisi katika usimamizi wa kazi na rasilimali, utekelezaji wa majukumu, kulinda haki na wajibu waajiri na wafanyakazi, kutoa ushauri kuhusu kujenga hali bora za kazi na maslahi na kusimamia haki na usatawi katika sehemu za kazi.

Akizungumzia utendaji kazi wa Wakala hiyo, Waziri Kairuki amesema kuwa hatakubali kuona Wakala hiyo kuwa ni sehemu ya tatizo kwenye utendaji kazi wa kila siku bali watumishi wafanye kazi kwa weledi na kuwa na mchango katika kuzipatia suluhisho changamoto zinazoikabili Serikali kwa sasa.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Dkt. Jabiri Bakari alipokuwa akimkaribisha Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma alisema kuwa ofisi yake inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ufinyu wa eneo la ofisi ambapo hadi sasa wanatumia gharama kubwa katika kukodisha jengo ili waweze kutimiza majukumu yao ipasavyo.Dkt Bakari alitaja changamoto nyingine kuwa ni ongezeko la tishio la usalama mtandaoni kutokana na ukweli kuwa kadiri Serikali inavyozidi kuhamia mtandaoni, hali ya uhalifu nayo inahamia mtandaoni.

Katika kutimiza majukumu yake, hadi sasa Wakala ya Serkali Mtandao ina wafanyakazi wapatao 94 ambapo inatarajiwa kuwa jumla ya watumishi 126 mara Serikali itakapotoa kibali cha kuajiri watumishi wapya.Wakala hiyo imejenga historia mpya ya kuwa na viongozi wa kwanza wa baraza hilo ambapo Donald Samwel amechaguliwa kuwa Katibu wa Baraza kwa kura 29 zilizopigwa za wajumbe wakati Dianah Mlokozi naye ameingia kwenye historia hiyo kwa kuchaguliwa kuwa Katibu Msaidizi wa baraza hilo.


Baraza la wafanyakazi la eGA limezinduliwa kwa mujibu wa kutekeleza Sera ya kuwakilisha wafanyakazi mahala pa kazi kkama ilivyoelekezwa kwenye sheria ya majadiliano katika utumishi wa Umma na sheria ya ajira na mahusiano kazini Na. 6 ya mwaka 2004.
k1 
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki akiongea na Watumishi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) (hawapo pichani) wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi kwenye ofisi za Wakala hiyo ziliopo Mtaa wa Samora, Jengo la Extelecoms mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.k2Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Dkt. Jabiri Bakari  akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki ili aweze kuzindua Baraza la Wafanyakazi kwenye ofisi za Wakala hiyo ziliopo Mtaa wa Samora, Jengo la Extelecoms mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairukik3Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Long’ida Oltetiai akitoa taarifa ya tawi hilo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi kwenye ofisi za Wakala hiyo ziliopo Mtaa wa Samora, Jengo la Extelecoms mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki.
k4 k6 
  Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi kwenye ofisi za Wakala hiyo ziliopo Mtaa wa Samora, Jengo la Extelecoms mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.k7 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) mara baada ya uzinduzi wa baraza hilo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.

No comments: