Friday, June 24, 2016

WANANCHI JIMBO LA KIKWAJUNI ZANZIBAR KUPATA HUDUMA YA MATIBABU BURE

Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wananchi wa Jimbo hilo wakati wa mkutano uliofanyika katika Ofisi ya Jimbo ambapo alitoa taarifa juu ya watu wazima kuanzia umri wa miaka 70 kupata huduma ya matibabu bure.
Wananchi wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati akizungumza katika mkutano uliofanyika katika Ofisi ya Jimbo ambapo alitoa taarifa juu ya watu wazima kuanzia umri wa miaka 70 kupata huduma ya matibabu bure.
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Tawi la Zanzibar, Ismail Kangeta, akitoa ufafanuzi juu ya huduma ya matibabu itakayoanza kutolewa bure kwa wananchi wa Jimbo la Kikwajuni, wakati wa mkutano uliofanyika Ofisi ya Jimbo.Wapili ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.
Mwananchi wa Jimbo la Kikwajuni akisoma kipeperushi kilichotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ambacho kina majina ya Hospitali ambazo wafaidika wa huduma ya matibabu bure wanaweza kwenda kupata huduma hiyo wakati wa mkutano uliofanyika Ofisi ya Jimbo hilo Kikwajuni Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia), akimsikiliza mmoja wa wananchi wa Jimbo hilo mara baada ya kutoa muda wa kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wakati wa mkutano uliofanyika Ofisi ya Jimbo hilo, Zanzibar.
Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni, Nassor Salim Jazeera (kulia), akimsikiliza mwananchi wa Jimbo hilo mara baada ya kutoa muda wa kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wakati wa mkutano uliofanyika Ofisi ya Jimbo hilo, Zanzibar.

No comments: