Thursday, June 9, 2016

SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAANZISHA SAFARI JIJI LA PERTH NCHINI AUSTRALIA KWA NDEGE YA BOEING 787-9 DREAMLINER.

Ndege ya uzinduzi ya Shirika la Ndege la Etihad ikipokelewa na magari ya zimamoto yaliyomwaga maji kuashiria uzinduzi rasmi wa Safari za ndege kati ya jiji la Perth Australia na Abudhabi. 

Ndege ya Shirika la Usafiri wa Anga la Etihad Boeing 787 Dreamliner imetua kwa mara ya kwanza katika Jiji la Perth nchini Australia baada ya kuzinduliwa kwa safari zake rasmi ikitokea Abu Dhabi.

Ndege ya Etihad EY486 iliondoka Abu Dhabi siku ya tarehe 02 Juni muda wa saa nne na nusu usiku na kuwasili Perth mji mkubwa uliopo magharibi mwa Australia saa saba na nusu mchana ambapo ilipokelewa rasmi kwa tamaduni za uzinduzi wa ndege mpya.

Ndege ya kurudi, EY487 iliondoka Perth saa 11 jioni na kuwasili Abu Dhabi saa sita na dakika 25 usiku wa tarehe 3 Juni.

Ndege hiyo ya B787-9 Dreamliner ya Etihad ni bora na kisasa kwa abiria kwa madaraja yote. Ina jumla ya viti 299 na ina uwezo zaidi ya asilimia 14 ukilinganisha na ndege ya Airbus A330-200. Kwa abiria wa daraja la juu, ni zaidi ya asilimia 27 kwa ubora wa viti vyake.

Makamu wa Rais wa Masoko wa Shirika la Ndege Etihad, Shane O’Hare alisema uamuzi wa kuleta ndege bora zaidi unaendana na umuhimu kibiashara baina ya Austaria Magharibi na shirika hilo.
 “Tangu tumezindua usafiri wa ndege kati ya Perth na Abu Dhabi miaka miwili iliyopita, tumefurahia kuhudumia watu wa madaraja tofauti kwa mafanikio.”

“Dreamliner imeongeza nafasi 518 kwa wiki katika safari za anga, jambo hili linatupa nafasi zaidi kuendana na mahitaji halisi ya wateja wetu.”

“Imewezesha pia wageni wetu kusafiri kwa raha mustarehe, huduma bora na ukarimu kutoka kwa wahudumu wetu wa Etihad.”

 “Ndege hiyo ya kisasa imeundwa kuendana na mahitaji mbalimbali ya weteja wetu, ikiwamo sehemu kubwa ambayo watapata viburudisho, pia ikiwa ni ndege bora zaidi kwa safari za mbali na karibu, huku huduma mbalimbali za burudani zikiwemo ndani ya ndege pamoja na huduma za kiwango cha juu.”

 “Bwana O’Hare aliongeza kuwa, “Kuanzishwa kwa huduma ya ndege ya Dreamliner kutawezesha kukuza utalii Magharibi mwa Australia.”

 “Kwa kuongeza safari za ndege kwa wiki Perth, Shirika letu la Etihad litakuwa chachu ya kuongeza ukuaji katika sekta ya utalii ambapo itawezesha watu mbalimbali kutoka ulimwenguni kote kutembelea hata wakati wa mapumziko.”

 “Kwa pamoja na washirika wetu wa masuala ya usafiri, tunatoa huduma za usafiri Ulaya, Mashariki ya Kati na ukanda wa kaskazini Marekani na hii sasa inatoa huduma bora kati ya Perth na Abu Dhabi.”

Ndege ya Etihad b787-9 iliyo katika kiwango cha juu ni matarajio itawahudumia watu wengi hapo baadaye ikiwa na vyumba maalumu  vilivyosheheni kila huduma kwenye daraja la kwanza 28 na viti 271 kwenye daraja la kati.

Katika daraja la kwanza kuna vyumba maalumu vyenye huduma zote muhimu vikiwa na nafasi ya kutosha pamoja na huduma ya kitanda. Pia, daraja la kwanza kuna mifumo mizuri ya ambayo itamwezesha abiria kusogeza kiti chake kadiri anavyopenda huku akiburudika na runinga ya kisasa pamoja na vifaa vya kuvaa masikioni vinavyomwezesha kupunguza kelele.
Aidha daraja la kati lenye viti 271 inampa mteja nafasi ya kupumzika kupitia kwenye kiti chake kwa namna kilivyotengenezwa ikiwa ni pamoja na kupata ya huduma ya runinga yake binafsi kwenye kiti chake.

Abiria akiwa kwenye Dreamliner atapata burudani ya muziki iliyounganishwa kwenye ndege hiyo. Huduma hiyo inapatikana kwa masaa yote uwapo kwenye ndege. Pia, kuna chaneli zinazorusha matangazo yake ya live huku zikiwa ni screen ambazo zina kiwango cha ubora wa hali ya juu huku zikimfanya abiria kujisikia vizuri.
Pia, hudma ya simu na wi-fe pamoja na sehemu za kuchomeka USB zinapatikana kwenye kila kiti.

Etihad limekuwa shirika linaloongoza kwa huduma bora zinazotolewa ndani ya ndege ikiwa na watoa huduma wenye uzoefu. Watoa huduma hao wana mafunzo ya kutosha kutoka kwenye vyuo vinavyotambulika kimataifa ambao watamsaidia abiria kila anapohitaji msaada hususani wale wanaosafiri na watoto.

Vyakula bora na salama vinavyopikwa na wataalamu kutoka hoteli maalumu, vinatolewa kwenye daraja la kwanza na wengine wanaweza kupata huduma hiyo kulingana na mahitaji ya abiria.

Shirika la Etihad ndilo shirika pekee linalotoa huduma ya usafiri kutoka magharibi mwa Australia na USA ikiunganisha na uwanja wa Ndege wa Abu Dhabi. Ipo huduma inayomwezesha mgeni kukamilisha masuala ya uhamiaji na ukaguzi wa kiusalama kwa USA wanaposafiri kwenda Abu Dhabi ili kupunguza usumbufu wanapowasili uwanja wa ndege wa Marekani.

Shirika la Etihad lilizindua safari za Airbus A330-200 Perth Julai 2014.

Tofauti na Perth, Shirika la Etihad pia linaunganisha zaidi ya miji 8 magharibi mwa Australia. Etihad imefanikiwa kuunganisha watu na miji ya Broome, Geraldton, Kalgoorlie-Boulder, Kununurra, Karratha, Paraburdoo, Port Hedland na Newman.

Vilevile Shirika la Etihad linatoa huduma katika mji wa Sydney ikiwa na safari mara mbili kwa siku ikiunganisha na Virgin Australia, pia mara mbili kwa siku Melbourne na mara mbili kwa siku mji wa Brisbane.

Perth ndiyo mji wa pili kwa ukubwa Australia unaohudumiwa na ndege ya kisasa ya Shirika la Etihad B787-9 Dreamliner na kwa mji wa Brisbane ilianza safari zake kwa mara ya kwanza Juni 2015.
Pia, ndege hiyo inatoa huduma Singapole, Washington DC, Zurich na Dusseldorf.

Vilevile Shirika linatarajia kuanzisha huduma hiyo Istabul, Johnnesburg na Shangai kwa kipindi hiki kilichobaki kwa mwaka huu.

Aidha ndege za Boing 787 Dreamliner inategemewa kuwa ndizo ndege zikazotoa huduma kwa miaka michache ijayo katika shirika hilo kutokana na ubora wake na teknolojia yake ya kisasa.

Wanaotumia ndege ya Dreamliner watafurahia usafiri huo kutokana na kuwa na madirisha makubwa, hewa nzuri ya ndani ya ndege, mandhari mazuri pamoja na vifaa vilivyopo ndani vyenye kutumia teknolojia ya kisasa.

Safari za  Abu Dhabi-Perth:

Namba ya Ndege
Inakotoka
Kuondoka
Mahali/kwenda
Kuwasili
Siku
Ndege
EY486
Abu Dhabi
(AUH)
4:30 usiku
Perth
(PER)
7:50 mchana next day
Daily
B787-9
EY487
Perth
(PER)
11:00 jioni
Abu Dhabi (AUH)
6:25 mchana
next day
Daily
B787-9

Muhimu: Muda wa kuondoka na kuwasili umewekwa kwa masaa ya eneo husika.

No comments: