Thursday, June 2, 2016

MGODI WA BUZWAGI WAKABIDHI HUNDI YA MILIONI 588 KWA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya Acacia, Mhandisi Asa Mwaipopo(wa kwanza kushoto) akikabidhi mfano hundi ya Sh Milioni 588,842,728 kwa mkuu wa wilaya ya Kahama, Mh Vita Kawawa(katikati) na Mwenyekiti wa Halmashuli ya Mji wa Kahama Mh Abel Shija (kulia) ikiwa ni sehemu ya pili ya ushuru wa huduma kuanzia Mwezi Julai – Desemba 2015 ambayo Kampuni hiyo imelipa kwa halmashauri ya mji Kahama.

Mkuu wa Wilaya Kahama, Vita Kawawa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Kahama wakikabidhi mfano wa Hundi ya Sh Milioni 5888,842,728 kwa mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kahama Anderson Msumba,fedha zilizotolewa na Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi kama ushuru wa Hudma (Service Levy) kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya kisasa .wengine pichani ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo (kushoto) akishuhudia tukio hilo. Watendaji wa Halmashauri ya mji wa Kahama nao wakiionyesha hundi hiyo mara baada ya kuipokea kutoka kwa mkurugenzi wa halmashauri. Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Vita Kawawa akiwahutubia baadhi ya wananchi (hawapo picha) na viongozi wakati wa hafla hiyo ya kupokea hundi kutoka kwa Mgodi wa Buzwagi. Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo akizungumza na viongozi na wananchi wa Kahama wakati wa hafla ya kukabidhi hundi hiyo.

Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kahama Anderson Msumba akitoa neo la shukrani mara baada ya kukabidhiwa hundi.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama,Vita Kawawa akiteta jambo na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya Acacia, Mhandisi Asa Mwaipopo wakati wa hafla ya kukabidhi Hundi hiyo.Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog Kanda ya Kaskazini.

Kahama: Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi umeikabidhi halmashauri ya mji wa Kahama hundi yenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni miatano themanini na nane ikiwa ni sehemu ya kodi ya huduma (service levy) katika kipindi cha kuanzia Julai – desemba 2015.

Akikabidhi hundi hiyo kwa mkuu wa wilaya ya Kahama, katika hafla fupi iliyofanyika katika uwanja wa taifa Kahama, Meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo amesema Kampuni yake imekuwa ikizingatia sheria kwa kulipa kodi mbalimbali ambazo zimewekwa kwa mujibu wa sheria.

“Toka kuanza kwa shughuli zetu za uchimbaji mwaka 2009 mpaka 2015 mgodi wa Buzwagi pekee umelipa kodi mbalimbali ambazo zinafikia kiasi cha shilingi za kitanzania bilioni 197 kiasi hiki kinahusisha kodi na tozo mbalimbali kama vile kodi ya huduma (service levy), Pay as you earn (PAYE), kodi ya zuio (withholding tax), na kodi ya mrabaha".alisema Mwaipopo.

"Katika kodi hizi, kodi ya huduma (service levy) imekuwa ikilipwa moja kwa moja kwa halmashauri ya mji wa Kahama ambapo mpaka mwisho wa mwaka jana zaidi ya shilingi bilioni 3.4 sawa na asilimia mbili ya kodi zote zimelipwa kwa halmashauri ya Kahama pekee.”aliongeza Mwaipopo.

Mwaipopo amesema licha ya Kampuni yake kulipa kodi mbalimbali bado imekuwa ikijishughulisha katika kuhakikisha inakuwa mdau muhimu wa maendeleo kwa kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yanayozunguka Mgodi.

“Mheshimiwa mkuu wa wilaya katika kipindi cha mwaka 2015 pekee takribani shilingi bilioni moja nukta saba 1.7 zimetumika katika kutekeleza miradi ya elimu, afya na maji na miradi yote hii ilelenga katika kuinua uchumi wa wilaya pamoja na kuboresha ustawi wa maisha ya wenyeji.”alisema Mwaipopo.

“Acacia kupitia Mgodi wetu wa Buzwagi tunajivunia kuwa mdau muhimu wa maendeleo kwa halmashauli ya mji wa Kahama na serikali kwa ujumla, na tunafarijika sana kwa ushirikiano ambao tumekuwa tukiupata.”

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Vita Kawawa aliyepokea hundi hiyo kutoka kwa uongozi wa Buzwagi na baadae kuikabidhi kwa mwenyekiti wa halmashauri ya Kahama ameupongeza uongozi wa Mgodi wa Buzwagi kwa jitihada ambazo wamekuwa wakizifanya katika kuhakikisha wanashirikiana na jamii katika kutekeleza miradi mbalimbali, huku akiwataka viongozi wa halmashauri ya mji wa Kahama kuhakikisha pesa hizo zinatumika kutekeleza miradi itakayokuwa na manufaa ya moja kwa moja kwa Jamii.

“Ombi langu kwa wataalamu wa halmashauri na madiwani ambao ndio wasimamizi wa pesa hizi kuhakikisha kuwa zinatumika kama zilivyokusudiwa na kwa sababu safari hii tumeamua zijenge hospitali basi hakikisheni tunapata majengo ya kisasa pamoja na vifaa tiba kwa manufaa ya watu wa Kahama”alisema Kawawa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Kahama Abel Shija amesema wao kama madiwani watahakikisha kwamba pesa hizo zinatumika katika utekelezaji wa miradi iliyokusudiwa.

“Ndugu zetu hawa wa Mgodi wamekuwa wakilipa kodi hizi lakini wananchi wamekuwa hawaoni kinachofanyika hali ambayo imepelekea minung’uniko miongoni mwa wananchi, Kwa kuamua kuzitumia fedha katika ujenzi wa Hospitali ya wilaya kila mtu ataona kinachofanyika na itasaidia kuondoa minunung’uniko ambayo imekuwa ikijitokeza kutoka kwa wananchi”

Hafla hiyo pia ilisindikizwa na burudani ya mpambano mkali wa mpira wa miguu baina ya timu za Mgodi wa Buzwagi na timu ya hospitali ya wilaya mchezo ambao uliisha kwa timu ya hospitali ya wilaya kuibuka mshindi kwa kuifunga timu ya Buzwagi 2-1.

No comments: