Wednesday, June 15, 2016

MAZOEZI YA YOGA KUFANYIKA MAY 19 MWAKA HUU KATIKA UFUKWE WA UFUKWE WA COCO BEACH.

 Balozi wa India hapa nchini, Sandeep Arya akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya watanzania wajitokeze  kwa wingi kufanya mazoezi siku ya Juni 19 mwaka huu kwenye ufukwe wa Coco beach jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa India hapa nchini, Sandeep Arya akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani)  nembo ya Yonga, leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya watu waliofika kufanya mazowezi ya Yoga, leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)

MAZOEZI ya viungo vya mwili yenye asili ya Indi nchiniIndia yanatarajia kufanyika Juni 19 mwaka huu katika viwanja vya ufukwe wa Cocobeach jijini Dar es Salaa ikiwa ni kuadhimisha siku ya Utamaduni wao na kimataifa kwa ujumla.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Balozi wa India hapa nchini, Sandeep Arya amesema kuwa Yogo ni mazoezi ya kiroho na kimwili yenye asili katika falsafa ya uhindi kwa mda wa miaka mingi.

Alimnukuu Waziri Mkuu wa India, Shri Narendra wakati akihutubia mkutano wake wa 69 wa Baraza Kuu la Umojawa Mataifa Septemba 27, 2014 alipendekeza jumuiya yakimataifa kupitisha siku ya Kimataifa ya Yoga.

Aidha ameeleza kuwa siku ya Yoga sio tu kufanya mazoezi bali mbinu ya kujitambua na kutambua mahusiano ya mtu na dunia na mazingira yake.

Balozi huyo amewaomba watanzania kujitokeza kwawingi kufanya mazoezi siku ya Juni 19 mwaka huu kwenye ufukwe wa Cocobeach Dar es Salaam huku akisemamazoezi ni uhai wa binadamu hivyo siku hiyo watawezakufundishwa mbinu mbalimbali za kufanya mazoezi yaviungo kutoka kwa wataalamu kutoka nchini India.

No comments: