Saturday, May 28, 2016

WABUNGE WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WATANGAZA RASMI KUMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI ,WAOMBA KUKUTANA NAE RASMI


  Mbunge Shyrose Bhanji wa Tanzania akichangia mada bungeni
 wabunge mbalimbali wakichangia mada bungeni wakati bunge la bajeti ya jumuiya ya afrika mashariki likiendelea
 wabunge wakijadiliana jambo wakati bunge likiendelea

Na Woinde Shizza,Arusha
Wabunge  wa bunge la Afrika mashariki wamesema kuwa wanamuunga mkono rais wa jamuhuri  ya Mungano wa Tanzania John Magufuli  na watampa ushirikiano katika kila jambo  kwani anafanyakazi kwa makini na vizuri . 
Pamoja na kumpongeza na kumuunga mkono Magufuli pia wameomba kukutana nae na kujadili baadhi ya mambo.

Wakiongea na waandishi wa habari wabunge baadhi ya wabunge hao walisema kuwa wanafurahishwa sana na kasi ya magufuli  kwani imekuwa na manufaa makubwa sio kwa watanzania pamoja na wananchi wa nchi za jumuiya ya afrika mashariki kwa ujumla.

 " kasi ya Rais Magufuli, imekuwa na manufaa makubwa sio kwa watanzania bali kwa wananchi wote wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki"alisema Mbunge Shyrose Bhanji wa Tanzania,

Aliongeza kuwa vita dhidi ya rushwa na ufisadi ambayo imeanzishwa na Rais Magufuli, ambaye pia ni mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, inapaswa kuungwa mkono na bunge hilo.

Mbunge Martin Ngoga wa Rwanda, alisema kasi ya Rais Magufuli ambaye ni mwenyekitiwa jumuiya hiyo,inapaswa kuungwa mkono na sio vibaya jumuiya ya Afrika ya Mashariki, kuonesha kwa dhati inapambana na rushwa.

"Rais Magufuli anafanyakazi nzuri sana na sisi kama wabunge tunamuuunga mkono ili kuwa na manufaa katika jumuiya ya Afrika ya Mashariki mataifa yote yanapaswa kushirikiana kuondoa rushwa"alisema

No comments: