Monday, May 23, 2016

Vijana wawili wajasiriamali wawezeshwa vitendea kazi baada ya kuudhuria mafunzo yaliyoandaliwa na Airtel FURSA

• Wawezeshwa vitendea kazi vyenye dhamani ya shilingi milioni tano.

Dar Es Salaam Mei 21, 2016, Airtel Tanzania inaendeleza dhamira yake ya kuendelea kuwashika mkono vijana hapa nchini  ambapo mwishoni mwa wiki hii kupitia mpango wake wa kutoa semina ya mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana ujulikanao kama Airtel FURSA Tunakuwezesha, uliweza kuchagua vijana wawili walioweza kuelezea na kuwakilisha changamoto wanazozipata katika biashara wanazozifanya mbele ya jopo la washauri ambao leo hii wamekabidhiwa  vitendea kazi vyenye dhamani ya shilling milioni 5  ili kuweza kukabiliana na changamoto hizo.

Akizungumza wakati wa sherehe ya makabidhiano hayo, Meneja wa Airtel huduma kwa Jamii Hawa Bayumi alisema "baada ya kufanya mafunzo ya biashara ya ujasiriamali wiki chache zilizopita na kuweza kufikia vijana zaidi ya 300 jijini Dar Es Salaam  waliojitokeza na kuzifahamu vyema FURSA zinazowazunguka ili kujitengenezea ajira na na uwezo wa kujenga fursa nyingine. Leo hii tupo hapa kuwawezesha hawa walioonyesha bidi zaidi”

“Na siku hiyo ilikuwa ni siku ya faraja kwani vijana waliweza kujifunza mambo mengi sana na mwisho wa siku waliweza kuelezea na kuwasilisha biashara zao mbele ya jopo la washauri na ulikuwa uamuzi mgumu sana lakini mwisho wa siku tuliweza kupata vijana wawili bora walioweza kushinda nyoyo za jopo la washauri hao, ambao leo  hii tupo hapa kwajili ya kuwakabidhi vifaa vyao ili waweze kwenda  kukabiliana na changamoto walizonazo katika biashara zao. "

 Mpaka sasa Airtel imefanya semina nyingi sana za mafunzo ya biashara ya ujasiriamli hapa nchini katika mikoa mbali mbali na kuweza kufikia vijana wapatao 4000. Lakini hii ni mara ya kwanza kwa  Airtel kufanya semina hiyo na hapo hapo kuchagua vijana wawili walioweza kuwezeshwa kwa kupatiwa vitendea kazi katika semina hiyo. 

Huu ni mfumo mpya ambao Airtel Fursa umeuanzisha kwani zaidi ya kuwapa elimu ya mafunzo ya biashara ya ujasiriamali vile vile watawezeshwa kuongezewa nguvu mali na kuimarisha biashara wanazozifanya. Airtel kupitia mpango wake wa Airtel FURSA itaendelea kutoa warsha hizi katika maeneo mbalimbali hapa nchini ili kuhakikisha inafikia vijana wengi zaidi.

Hivyo tunawahamasisha  vijana wanaposikia nafasi kama hii popote walipo , kuchangamkia kwa kuhudhuria kwani  elimu inayotolewa  ni bure kabisa bila gharama yoyote. "aliongeza Bayumi.

Nae kwa upande wake  kijana Stephen Gimase, mmoja wa vijana aliyeshinda kwa kuweza    kuelezea na kuwakilisha changamoto anazozipata katika biashara waliyonayo mbele ya jopo la washauri wiki chache zilizopita katika mafunzo hayo, anayejishughulisha na shughuli za kutotoa vifaranga vya kuku,  alisema ,”naishukuru sana Airtel kwa kunipatia vifaa vya kisasa kwa ajili ya biashara yangu. Naahidii  kuwa nitafanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha nakuza biashara yangu na kujenga ajira kwa vijana wengine hapa nchini. Hii ni atua ya kwanza ya mafanikio ya maisha yangu nawashukuru Airtel kwa kuwa sehemu ya maisha safari yangu ya mafanikio "alisema Stephen.

Kijana mwingine aliyeweza kupata bahati ya kuwezeshwa na Airtel FURSA katika mafunzo hayo  ni msanii wa kuchora picha, Theresia Maliatabu ambaye amewezeshwa kwa kupatiwa vitendea kazi kwa ajili ya kuendeleza biashara yake kwa kupatiwa kompyuta na ubao wa kisasa wa kuchorea picha zake . Wakati wa sherehe ya makabidhiano hayo , Theresia aliwashukuru Airtel kwa kuweza kumshika mkono , na kuahidi kwamba ataifanya kazi yake kwa ubora zaidi na kuweza kufikia ndoto yake ya kuwa mchoraji bora na maarufu hapa nchini na hata nje tya nchi.

Tunaamini kwamba kupitia mpango huu wa mafunzo ya biashara ya ujasiriamali yanayotolewa na Airtel Fursa tunaamini vijana wengi watatoka na kukimbilia mafunzo haya kwani watakuwa wameweza kunufaika na kupata mafunzo haya katika nyanja mbali mbali za kuwawezesha kuanzisha na wengine kuweza kuendeleza biashara zao kwa njia ya ufanisi zaidi.
 Stephen Gimase (Kulia) ambaye ni miongoni wa vijana waliowezeshwa na mpango wa Airtel FURSA “Tunakuwezesha” akiangalia vifaa alivyokabidhiwa na Airtel FURSA kwa ajili ya kuboresha biashara yake ya kutengeneza mashine za kutengenezea vifaranga vya kuku, Kushoto ni Meneja wa huduma za jamii wa Airtel, Hawa Bayumi 
Meneja wa huduma za jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (2 Kushoto) akimkabidhi Theresia Maliatabu (Kulia) ambaye ni miongoni wa vijana waliowezeshwa na mpango wa Airtel FURSA “Tunakuwezesha” vifaa vyakuboresha biashara yake ya uchoraji ikiwemo meza ya kuchorea na kompyuta ya kisasa. Kijana huyu Aliyechaguliwa kutoka kwenye mafunzo ya biashara ya ujasiriamali  ya Airtel FURSA yaliyofanyika Dar es Salaam wiki chache zilizopita. Akishuhudiwa na mama yake mzazi Judith Benedicto (Katikati) na mama mkubwa Salome Benedicto (Kulia) pamoja na Afisa mauzo wa Airtel katika hafla iliyofanyika Mbagala kuu, jijini Dar es Salaam.

No comments: