Tuesday, May 3, 2016

UMOJA NA MSHIKAMANO NDIO SIRI YA MAFANIKIO BARA LA AFRIKA – NDUGAI

Na Owen Mwandumbya, Midrand Afrika Kusini.

Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai amesema ili Bara la afrika liweze kuwa Bara lenye nguvu kiuchumi na sauti ya maamuzi duniani halina budi kujikita katika umoja na mshikamono.

Mhe. Ndugai aliyasema hayo alipokuwa akilihutubia Bunge la Afrika (Pan African Parliament) leo kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa Bunge hilo wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo uliofanyika Mjini Midrand Afrika Kusini.

Akizungumzia changamoto zinazolikabli bara la Afrika Mhe. Nduagi alisema nchi nyingi barani Afrika zinakabiliwa na matatizo yanayolingana ambayo ni Vita vya wenyewe kwa wenyewe, ugaidi, umasikini na mengineyo ambayo yanahitaji suluhisho la Pamoja kuyakabili..

“ katika duniani ya sasa ni vyema tukakabiliana na changamoto zinazotukabili kwa pamoja. Matajiri hawawezi kuepuka athari za umasikini na ukosefu wa amani. Kinachotokea eneo moja kinaathiri maeneno mengi mathalani vita vya wenyewe kwa wenyewe Somalia imesababisha wakimbizi katika maeneo mengi duniani” alisema Ndugai

Akizungumzia nafasi ya wabunge katika kupiga vita changamoto zinazolikabili bara la Afrika, Mhe. Ndugai amesema wabunge wa Bunge la Afrika kama wawakilishi wa Manbunge ya Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika wanawajibu wa kutetea maslahi ya Bara la Afrika bila kujali itikadi za kisiasa, maeneo wanayotoka na mambo mengine yanayoweza kuligawa bara la Afrika.

“ Mkiwa Wabunge mnaowakilisha nchi zenu katika Bunge hili, nilazima mhakikishe Umoja wa Afrika unasimamia ipasavyo masalahi ya bara la Afrika ili kutimiza ndoto waliokuwa nayo waasisi wa umoja huu wa Afrika. Kwa mfano baba wa Taifa la Tanzania Mwalimu Julius kambarage Nyerere alisema lazima tukimbie wakati wengine wakitembea” aliongeza Ndugai

Mapema akitoa salamu za Bunge la Lesotho, Spika wa Bunge la Nchi hiyo Mhe. Nthloi Motsamai alisifu juhudi za Mwalimu Julius Nyerere pamoja na waasisi wengine wa bara hili katika kuimarisha umoja wa Afrika na kuwataka wabunge wa Bunge la afrika kuhakikisha mawazo ya viongozi hawa ya kulifanya bara la afrika kuwa moja yanatimia.

Katika hatua nyingine, wabunge wa Tanzania wanaowakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika walikula kiapo cha uaminifu kuwa wabunge wa Bunge hilo baada ya Bunge la Tanzania kuwachagua mapema mwezi Januari.

Wabunge hao ni pamoja na Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile, Mhe. Mboni Mhita, Mhe. David Silinde na Mhe. Asha Abdalah Juma. Mhe. Ndugai anatarajia kurejea nchini kesho jumatano ambapo Bunge la Afrika linaendelea na Vikao vyake hadi tarehe 13 Mei, 2016.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akilihutubia Bunge la Afrika (Pan African Parliament) kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa Bunge hilo wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo uliofanyika Mjini Midrand Afrika Kusini. Mhe. Ndugai alikuwa miongoni mwa viongozi mashuhuri 12 kutoka Barani Afrika walioalikwa kutoa ujumbe huo kwa wabunge wa Afrika.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akilihutubia Bunge la Afrika (Pan African Parliament) kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa Bunge hilo wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo uliofanyika Mjini Midrand Afrika Kusini. Mhe. Ndugai alikuwa miongoni mwa viongozi mashuhuri 12 kutoka Barani Afrika walioalikwa kutoa ujumbe huo kwa wabunge wa Afrika.
Spika wa Mhe. Job Ndugai akiwa na baadhi ya Maspika wenzie kutoka mabunge ya Nchi za Bara la Afrika kwenye Mkutano wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament) alikoalikwa kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa Bunge hilo wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo uliofanyika Mjini Midrand Afrika Kusini. Mhe. Ndugai alikuwa miongoni mwa viongozi mashuhuri 12 kutoka Barani Afrika walioalikwa kutoa ujumbe huo kwa wabunge wa Afrika. Kulia kwake ni Spika wa Bunge la Seneta la Lesotho Mhe Seeiso Berenge Seeiso na kushoto ni senate kutoka Bunge la Afrika Mhe. Bennette hayatoe
Wabunge wa Bunge la Afrika wanaowakilisha Tanzania wakila kiapa cha uaminifu. Kutoka kushoto ni Mhe. Asha Abdalah Juma, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile, Mhe. David Silinde na Mhe. Mboni Mhita.
 

No comments: