Saturday, May 14, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV; Waziri wa viwanda biashara na uwekezaji Charles Mwijage amesema serikali itawachukulia hatua kali wale watakaobainika kuwaibia wakulima kwa kutumia mizani mibovu; https://youtu.be/QpdZ3ZGoVw8

SIMU.TV; Ukosefu wa madawati katika shule za msingi za Juhudi na Ilemi katika jiji la Mbeya lasababisha msongamano mkubwa kwa wanafunzi;https://youtu.be/yvTo8PheJpA

SIMU.TV; Mafundi magari kutoka Tegeta wilayani Kinondoni mkoani Dar es salaam wajitolea kuchangia madawati 100 ili kuunga mkono jitihada za rais Magufuli;https://youtu.be/_9zLA1KFHJ0

SIMU.TV; Mkuu wa wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara Emmanuel Luhahula amewakamata viongozi 26 wa vyama vya msingi kwa kutokuwalipa wakulima fedha zao; https://youtu.be/khp8ELHUm84

SIMU.TV; Serikali za kusini mwa bara la Afrika zashauriwa kutenga fedha za kutosha ili kuboresha sekta ya kilimo; https://youtu.be/EjAuQ1YQV7k

SIMU.TV; Sekta ya mawasiliano nchini yajivunia kuchangia asilimia 3.6 ya pato la taifa kwa mwaka wa fedha 2015/2016; https://youtu.be/kWOuB761LXQ

SIMU.TV; Faida ghafi ya kampuni ya Tanga Cement imeshuka kutokana na kudorora kwa uzalishaji hali ilioyosababishwa na kukatika katika kwa umeme;https://youtu.be/UMv9frztvPU  

SIMU.TV; Ligi kuu bara inatarajia kuendelea katika viwanja tofauti huku jicho la wengi litakuwa uwanja wa taifa katika mchezo kati ya Ndanda na Yanga, huku wakitegemea kukabidhiwa kombe lao; https://youtu.be/zzygfBae9L4

SIMU.TV; Mabondia kutoka nje ya Tanzania wameomba mareferee kutoa maamuzi kwa kuzingatia sheria na haki huku wakiombwa kuweka kando uzalendo;https://youtu.be/PoH-GZlMaCA

SIMU.TV; Wanafunzi wanaoshiriki michezo ya Umitashuta wakabidhiwa vifaa vya michezo kutoka kwa diwani wa kawe Mwita Lwakatare na kuwaomba warudi na ushindi; https://youtu.be/H9z1Ws2U3KE   

SIMU.TV; Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ameiagiza wizara ya ujenzi mawasiliano na uchukuzi kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuchukua hatua za mara moja kuhakikisha inatatua dosari zilizopo kwenye vifaa vya ukaguzi katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.https://youtu.be/u_NdHkZ5tho   

SIMU.TV; Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa viongozi wakuu wa nchi walioshiriki mkutano wa kimataifa wa kupambana na rushwa wamevutiwa na jitihada zinazochukuliwa na Tanzania katika kupambana na rushwa.https://youtu.be/96pkkElm6A0  

SIMU.TV; Mafundi  gereji kutoka mtaa wa Tegeta Mageraji wameunga mkono kampeni ya kuchangia madawati katika shule za Dar es Salaam kwa kuchangia madawati 100.https://youtu.be/G2bC9U0bwJ8  

SIMU.TV; Sakata la sukari pamoja na operesheni ya kutafuta walioficha bidhaa hiyo limemuibua aliekua mwenyekiti wa CUF Profesa Lipumba na kuishauri serikali kusitisha zoezi hilo. https://youtu.be/d5A8ZvxKoWc  

SIMU.TV; Ukosefu wa mashine za X ray na Ultra sound katika hospitali ya wilaya ya Nyamagana ni mojawapo ya changamoto zinazoikabili hospitali hiyo.https://youtu.be/Wv2ZpdhIBXE  

SIMU.TV; Wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga katika eneo la kariakoo wamejikuta wakitawanywa na mabomu ya machozi baada ya kutaka kuzuia msafara wa rais akitokea uwanja wa ndege ili wamueleze kero zao.https://youtu.be/ZSYNdbB_Xto  

SIMU.TV; Baadhi ya wananchi katika eneo la Tazara jijini Dar es Salaam wamepomgeza juhudi za serikali katika kutekeleza mradi wa barabara ya juu katika eneo la Tazara yaani fly over. https://youtu.be/Hg7Z0RQ5Y3g  

SIMU.TV; Mahakama imetoa hukumu ya kugombea maiti kati wa wazazi wa mtoto David Shukuru ambapo wazazi walikuwa wakigombania kumzika kwa dini ya kiislam au kikristo. https://youtu.be/40811JgQ7hE  

SIMU.TV; Sekta ya mawasiliano imekua ya pili kwa ukuaji hapa nchini pamoja na kuwa mbele katika kuchangia pato la taifa. https://youtu.be/V03GnwR3q5M  

SIMU.TV; Benki ya CRDB imehimiza wateja wake kutumia huduma ya Internet Banking inayowawezesha wateja wake kupata huduma za kibenki popote walipo.https://youtu.be/7w2sMJeUKlw  

SIMU.TV; Kocha mkuu wa timu ya taifa Taifa Stars mei 18 anatarajia kutangaza kikosi kitakachocheza mchezo wa kirafiki na timu ya Kenya huko jijini Nairobi.https://youtu.be/FgiHD0quUHc  

SIMU.TV; Waziri wa kilimo na uvuvi Mheshimiwa Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa kesho wa Yanga dhidi ya Ndanda ambapo atakabidhi kombe la ligi kuu kwa washindi wa ligi hiyo timu ya Yanga.https://youtu.be/E4rq4Vq_7vo

SIMU.TV; Kikosi cha Mbeya City kimetua mkoani Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa lala salama dhidi ya Mwadui fc. https://youtu.be/-I_T3TMZoTY

SIMU.TV; Waalimu wanaofundisha michezo kwenye shule za sekondari na msingi wilaya ya Geita wameiomba serikali kuwapa motisha katika kutekeleza jukumu ilo.https://youtu.be/gTgOOvIStTY  

SIMU.TV; Bondia Thomas Mashali kesho anategemea kupambana na mpizani wake kutoka nchini Iran. https://youtu.be/7j5KxCLSwxU
  
SIMU.TV; Mshambuliaji wa klabu ya PSG ya nchini Ufaransa ataondoka mwishoni mwa msimu huu ambapo anatarajiwa kujiunga na ama klabu ya Manchester United au kutimukia nchini Marekani. https://youtu.be/xgKk2i8LlYU

No comments: