Sunday, May 29, 2016

SERIKALI YATAKIWA KUFUNGUA OFISI ZA UTALII KATIKA NCHI AMBAZO ZINALETA WATALII WENGI HAPANCHINI

Serikali imetakiwa kufungua ofisi za utalii katika kila nchi ambazo zinaleta watalii hapa nchini pamoja na kupunguza viingilio vya wageni wanaotembelea hifadhi zetu za taifa ili kuweza kuongeza idadi ya watalii wanaoingia hapa nchini .

Hayo yamebainishwa na Mbunge wa jimbo la Arumeru magharibi Gibson Olemeiseyeki wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari alipotembelea katika maonyesho ya utalii ya Karibu fair yanayofanyika ndani ya viwanja ya magereza, jijini Arusha .
wananchi wakiendelea kupata maelezo ya utalii ndani ya banda la Ngorongoro Conservation lililopondani ya maonyesho hayo.

Alisema kuwa serekali inapaswa kufungua ofisi katika kila nchi ambayo inaleta wageni hapa nchini ili kuweza kutangaza utalii wetu vizuri, na ili kuweza kupata wageni wengi zaidi ambapo wakiingia kwa wingi watasaidia kuongeza pato la taifa na kupunguza tatizo la ajira kwani vijana wengi wanaweza kujiajiri kupitia utalii pamoja na biashara za utalii .

Alibainisha kuwa ni jambo la ajabu nchi kama Tanzania ambayo inavivutio vingi vya utalii huku ikiwa ni nchi mojawapo ambayo iko katika nchi kumi bora ambazo zinaongoza kwa kuwa na vivutio vya utalii lakini ni nchi ambayo inaongiza watalii wachache sana ukilinganisha na vivutio vilivyopo.

“nchi kama Tanzania pamoja na vivutio vyote lakini kwa mwaka tunaingiza watalii milioni moja wakati nchi kama Malaysia kwa mwaka wanaingiza watalii miolini 15 ni jambo la kushangaza alafu ukiwaangalia viongozi wetu badala ya kukaa na kuangalia jinsi ya kufanya ili wataliii waingie na wawe wengi lakini wao wanakaa wanachekelea na wanafanyakazi ya kuongeza ada ya kuingia katika hifadhi zetu kila mara, sasa hii kweli si itakimbiza wageni badala ya kufanya wageni waongezeke kila siku”alisema Olemeiseyeki.
Mbunge wa jimbo la Arumeru magharibi Gibson Olemeiseyeki akipata maelekezo ya huduma zinazotolewa na kampuni ya utalii OSUPUKO nature Paradise iliopo mkoani Arusha.

Alisema kuwa kupitia utalii serekali inaweza kuingiza fedha nyingi sana na  pia inaweza kuwaajiri vijana wengi sana, iwapo ikijipanga vizuri na kutumia fursa vizuri kwani kama nchi zingine zinaweza hata serekali yetu itaweza iwapo tu itaajiri wafanyakazi ambao wanauchungu na hifadhi zetu na pia wanataaluma ya kutosha kuhusiana na utalii na sio kuajiri watu ambao hawana taaluma na kuajiri watu kiundugu undugu na kiubinamu.
Meneja wa Banki ya ABC Joyce Malai akiwa anawapa maelezo ya huduma zinazopatikana katika benki yao na jinsi ya kufungua akaunti ndani ya benki yao ambapo alisema kuwa kima cha chini cha kufungulia akaunti ndani ya benki yao ni shilingi 5000 na benki yao inatoa huduma ndani ya nchi na nje kwani ni ya VISA na pia unaweza kulipia kitu chochote ukiwa na kadi yao ATM card.

Aidha alimalizia kwa kuitaka serekali kupunguza tozo za utalii pamoja na kurahisisha ujaji wa wageni hapa nchini ili kuweza kukuza ongezeko la watalii nchini pamoja na kuboresha miundombinu ndani ya hifadhi zetu.

Kwa upande wa afisa uhusiano wa chama cha waajiri nchini (ATE), Patricia Chao alisema kuwa maonyesho ni mazuri na kwani muamko upo, watu wamehudhuria kwa wingi tofauti na kipindi kingine kwani amewaona washiriki wengi kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na hata Afrika Kusini tofauti na kipindi kingine.
Afisa usiano wa chama cha waajiri (ATE) Patricia Chao akiwapa maelekezo baadhi ya wateja wakigeni waliouthuria katika banda lao kujua jinsi ili kuweza kujua jinsi chama cha waajiri kinavyofanya kazi.

Emma Saria Treasury Dealer wa benki ya ABC akiwa anawaonyesha wateja waliouthuria katika banda lao aina tofauti tofauti za kadi za benki zinazotolewa na banki yao.
kikundi cha ngoma kikiendelea kutumbuiza.
wamama wa kimasai wakiwa wamekaa wanaangalia burudani mbalimbali za vikundi vya ngoma.
 kikundi cha ngoma kutoka morogoro kikiendelea kutumbuiza ndani ya baadhi ya mabanda yalikuwepo katika maonyesho. Habari picha na Woinde Shizza,Arusha

No comments: