Tuesday, May 24, 2016

SEKTA YA NGOZI INA NUKSI- PROFESA MKENDA.

Katibu wa Wizara ya Viwanda na Uwekezaji-Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda  (Mwenye suti)akipewa maelekezo na Katibu Mwenezi wa Chama cha Wanunuzi wa Ngozi Tanzania (Wangota) juu hali biashara ya ngozi inavyodorola leo jijini Dar es Salaam. 
 Katibu wa Wizara ya Viwanda na Uwekezaji-Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda (Mwenye Suti)   akioyeshwa ngozi na zilizoahifadhiwa na katika  Maghala ya Ngozi leo jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Wizara ya Viwanda na Uwekezaji-Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda akiangalia ngozi ambazo zimehifadhiwa katika maghala ya kuhifadhi ngozi leo jijini Dar es Salaam.
Ngozi ambazo zimehifadhiwa katika maghala ya Ngozi  Vingunguti jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii)

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
SEKTA ya Ngozi imekuwa na Nuksi kutokana na baadhi ya viwanda vya ngozi kufungwa huku wamiliki wa maghala ya ngozi wanalia na biashara hiyo kuwa haitoki hata ikitoka wanauza kwa hasara.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Uwekezaji-Uwekezaji, Profesa, Adolf Mkenda wakati alipotembelea maghala ya ngozi , Profesa Mkenda amesema kuwa serikali itahakikisha inaweka mazingira bora ya wafanyabiasharaya ngozi kuweza ngozi hiyo kuzalisha bidhaa za ngozi kuuzwa ndani na sio kupeleka nje ya nchi.

Mkenda amesema kuwa katika mazingira wanayoweka ni kuhakikisha wawekezaji wa ndani ndio wanamiliki sekta hiyo na sio kutegemea watu wa nje ya nchi ambao wakati wote anakuwa na hati ya kusafiria kurudi kwao baada ya kuona biashara inadorola.

Amesema kuwa kuna kiwanda kimefungwa Shinyanga kutokana na kukosa malighafi ya ngozi huku baadhi ya maghala ya Dar es Salaam yakiwa na ngozi iliyokaa kwa muda wa miaka miwili.

Mmoja wa Wamiliki wa Maghala ya Ngozi, Omary Msangi amesema kuwa viwanda vilivyopo ngozi vinunua ngozi kwa bei ndogo huku gharama za kuhifadhi ngozi ikiwa kubwa.

No comments: