Saturday, May 28, 2016

msimu mpya wa Maisha Plus East Africa 2016 waanza rasmi, sasa kurushwa kupitia Azam TV


Muanzilishi wa Maisha Plus, Masoud Kipanya akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa msimu mpya wa kipindi hicho, uliofanyika jana usiku katika viwanja vya Studio za Azam Tv na kutegemewa kuanza kuonyeshwa mapema jumapili hii saa tatu usiku katika channel ya Azam Two.Na kauli mbiu ya mwaka huu ni #HAPA KAZI TU.

Muanzilishi wa Maisha Plus, Masoud Kipanya akifurahi jambo na washiriki wa vipindi vilivyopita vya Maisha plus wakati wa hafla ya ufunguzii uliofanyika katika viwanja vya Studio za Azam Tv na kutegemewa kuanza kuonyeshwa mapema jumapili hii saa tatu usiku katika channel ya Azam Two.Na kauli mbiu ya mwaka huu ni #HAPA KAZI TU.

Wasanii Vitali Maembe na Jhikoman wakitoa burudani katika uzinduzi huo.

Mwanahabari na bloger John Bukuku akihojiwa na mtangazaji wa Azam Tv Benerick ambaye pia alikuwa ni mmoja wa washiriki wa msimu uliopita wa maisha plus.

Waanzilishi wenza wa kipindi cha Maisha plus Kaka Bonda na David Sevuri wakifurahia jambo wakati wa ufunguzi rasmi wa kipindi cha maisha plus mapema jana usiku katika viwanja vya studio za Azam Tv.

Mmoja wa washiriki wa msimu uliopita wa vipindi vya maisha plus akihojiwa na mtangazaji wa Azam wakati wa ufunguzi wa msimu mpya wa Maisha plus East Afrika 2016 yenye kauli mbiu ya #HAPA KAZI TU.

Mkurugenzi wa Azam Media,  Tido Mhando (Kushoto) akiwa na Masoud Kipanya akiongea na wageni waaalikwa waliohudhuriia uzinduzi wa Maisha Plus East Africa 2016 ambaye itaoneshwa katika chaneli ya Azam TWo kuanzia jumapili hii saa tatu usiku.

Baadhi ya wafanyakazi wa Azam Media wakishuhudia ufunguzi rasmi wa msimu mpya wa Maisha plus East Afrika 2016 yenye kauli mbiu ya #HAPA KAZI TU.

Wawakilishi kutoka bodi ya filamu Tanzania wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa Maisha Plus East Africa 2016 uliofanyika jana katika viwanja vya studio za Azam Tv.

Aliyekuwa mshindi wa kwanza wa Maisha Plus Abdul akizungumza katika uzinduzi huo.

Baadhi ya wageni waalikwa waliofika jana katika uzinduzi wa maisha plus wakifuatilia kwa makini

No comments: