Thursday, May 19, 2016

MeTL Group yatoa msaada wa Mil. 30.7 kwa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili

Mkuu wa Shule ya Tiba katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS), Prof. Slyvia Kaaya (wa nne kulia) akizungumza machache kabla ya kukabidhiwa rasmi viti 200 na uongozi wa kampuni ya MeTL. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Kampuni ya MeTL, Murtaza Dewji.

Kwa kutambua umuhimu wa elimu, kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) imetoa msaada wa Milioni 30.7 kwa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) ili kusaidia ununuzi wa viti 200 ambavyo vitatumiwa na wanafunzi wa udaktari wa watoto.

Akizungumza na Modewjiblog kuhusu msaada huo, Mkuu wa Shule ya Tiba katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS), Prof. Slyvia Kaaya, amesema kabla ya kupata msaada huo walikuwa wakitumia chumba kidogo ambacho kilikuwa hakiwatoshi wanafunzi wanaosomea udaktari wa watoto hivyo msaada huo umekuwa muhimu kwao ili kupunguza changamoto ambazo zinawakabili.

“Msaada huu utatusaidia sana na hata sasa hivi tuna matarajio tutakuwa na matokeo mazuri kwa kuongezeka kwa watahiniwa, wanafunzi kuhudhuria vipindi na hata kwa walimu uadilifu wa kufundisha utaongezeka,” alisema Prof. Kaaya.

Aidha Prof. Kaaya alisema pamoja na msaada huo lakini bado wanachangamoto ambazo zinawakabili ambazo zinahitaji kutafutiwa ufumbuzi ikiwa ni pamoja na kufunga viyoyozi na kuweka mitambo ya kuzuia mwangwi ili kuwawezesha wanafunzi kusoma bila kuwa na matatizo.

Nae Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer alisema kampuni yao imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kwa jamii ili kusaidiana na serikali kumaliza baadhi ya changamoto zilizopo na wamejipanga kuendelea kuwa wakitoa misaada kwa wahitaji.

“Tunaamini elimu ni muhimu kwa maendeleo ya baadae tunatoa msaada ili wasome na wawasaidie wengine kupitia elimu wanayoipata chuoni,” alisema Fatema Dewji-Jaffer.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Kampuni ya MeTL, Murtaza Dewji (kushoto) akitoa salamu za kampuni ya MeTL kabla ya kukabidhi viti 200 kwa uongozi wa MUHAS. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL, Fatema Dewji-Jaffer.
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL), Fatema Dewji -Jaffer (wa tatu kulia) akimkabidhi moja kati ya viti 200 Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS), Prof. Aporinal Kamuhangwa (wa pili kushoto) vilivyotolewa na kampuni ya MeTL Group. Kushoto ni Mkuu wa Shule ya Tiba katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS), Prof. Slyvia Kaaya. Wengine wanaoshuhudia tukio hilo kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa kampuni ya MeTL Group, Murtaza Dewji na Meneja Mwendeshaji wa Mo Dewji Foundation, Barbara Gonzalez (kulia). Mstari wa nyumba ni watumishi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba (MUHAS).
Picha ya pamoja baada ya makabidhiano yaliyofanyika katika jengo la Watoto lililopo Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS), Prof. Aporinal Kamuhangwa akitoa shukrani kwa Mkurugenzi wa Uendeshaji wa kampuni ya MeTL Group, Murtaza Dewji baada ya kukabidhiwa viti hivyo.
Meneja Mwendeshaji wa Mo Dewji Foundation, Barbara Gonzalez (kulia) akizungumza neno baada ya hafla fupi ya kukabidhi viti hivyo.
Uongozi wa MeTL na MUHAS wakiwa wamekaa kwenye viti hivyo.
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL), Fatema Dewji -Jaffer (katikati) akifurahi jambo na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa kampuni ya MeTL Group, Murtaza Dewji. Kushoto ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS), Karim Manji.
Viti 200 vya MUHAS vilivyotolewa na Kampuni MeTL.

No comments: