Monday, May 30, 2016

Maadhimisho Siku ya Hedhi Salama Duniani; Wadau watuma salamu kwa Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu.

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi (wa kwanza kushoto )akimsikiliza kwa umakini mmoja wa wadau wa agenda ya Hedhi salama nchini alipokuwa akitembelea vibanda vya maonyesho ya wadau hao kwenye viwanja vya mnazi mmoja  wakati Maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi (wa pili kulia )akimsikiliza kwa umakini mmoja wa wadau wa agenda ya Hedhi salama nchini alipokuwa akitembelea vibanda vya maonyesho ya wadau hao kwenye viwanja vya mnazi mmoja  wakati Maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
 WADAU wakiwa katika picha ya pamoja na wadau hedhi salama hapa nchini  wakiwemo wawakilishi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Wizara ya Afya,  kampuni ya Kasole Secrets Company pamoja na wadau wengine wa Elimu na Usafi wa Mazingira yakiwemo mashirika ya ACRA, WSSCC, SAWA, UNICEF, WaterAid, GIZ, SNV, Plan International, Flaviana Matata Foundation, Msichana Initiative, JALI INTERNATIONAL, FLAVIANA MATATA FOUNDATION, MSICHANA INITIATIVE, JALI Project, TAYOA,  VIGOR na TMARC Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi (katikati)aliemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw Paul Makonda  wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Baadhi ya wasanii maarufu nchini, Kajala Masanja na Queen Darleen (wenye fulana nyeusi) wakiwa pamoja na wanafunzi kutoka shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam wakati wa maandamano ya kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi (wa pili kulia )akimsikiliza kwa umakini mmoja wa wadau wa agenda ya Hedhi salama nchini alipokuwa akitembelea vibanda vya maonyesho ya wadau hao kwenye viwanja vya mnazi mmoja wakati Maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 

Na Mwandishi wetu.
WADAU wa kutetea agenda ya hedhi salama hapa nchini wamemuomba Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu  kutetea vikali  masuala yanayohusu  hedhi salama ikiwemo  uwepo wa mitaala ya elimu iliyo wazi juu ya hedhi salama na usafi kipindi cha hedhi katika shule zote za Msingi na Sekondari hapa nchini.


Wadau hao walitoa ombi hilo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi aliemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw Paul Makonda  wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Kupitia risala iliyoandaliwa na wadau hao na kusomwa na mmoja wa wanafunzi, Halima Akida Mwanafunzi shule ya msingi Tandale wadau hao walimuomba makamu wa Rais Mama Samia Suluhu apiganie kuona kwamba masomo yanayofundishwa mashuleni kuanzia darasa la nne yanajumuisha elimu ya kina juu ya hedhi salama na usafi kipindi cha hedhi ikiambatana na mazingira sahihi ya usafi wa vyoo bora ili kuleta mchango mkubwa katika kunyanyua ubora wa elimu ya mtoto wa kike nchini.

“Vilevile, ipo haja ya kuwepo kwa uwezeshwaji mkubwa baina ya Wizara zote ambazo zina dhamana kubwa katika masuala ya Jinsia, Elimu, Afya, Ardhi na Maji. Pamoja na wadau wa maendeleo ambao wanamaslahi katika suala la upatikanaji wa maji safi na salama na usafi wa vyoo bora, ili waweze kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja,’’ aliongeza mwanafunzi
Aidha wadau  hao waliongeza kuwa kuna haja ya  kufanya marekebisho ya sheria ya kodi kwa kuondoa Ongezo la Kodi ya Thamani (VAT) katika bidhaa zote zinazohusiana na usafi wa ndani wa mwanamke.

“Kwa kuzingatia unyeti wa uharaka na athari chanya za suala hili, tunatoa wito kwa suala hili kupewa nafasi na kujadiliwa katika Mkutano wa Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaoendelea mkoani Dodoma,’’ aliongeza. 

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi alisema tayari serikali imeanza kuoangalia  ni jinsi gani itazileta pamoja TAMISEMI na Wizara tatu, ambazo ni Wizara ya Maji, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ili kufahamu namna zinavyoweza kutengeneza nia ya pamoja katika kutafuta suluhusho la kudumu.

“Aidha Serikali itahimiza wananchi kupitia kamati za shule kuanzisha mfuko maalumu katika shule zote nchini ambao utasimamia mahitaji yote ya lazima yanayohusu maji na usafi wa mazingira mashuleni,’’ alibainisha.

Zaidi Bw Mushi aliwapongeza wadau wao ikiwemo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Wizara ya Afya kwa kushikirikiana na kampuni ya Kasole Secrets Company pamoja na wadau wengine wa Elimu na Usafi wa Mazingira kwa kuandaa na kuadhimisha maadhimisho hayo kwa miaka miwili mfululizo kwa mkoa wa Dar es Saalam na kwa ngazi ya kitaifa.

Wadau hao ni pamoja mashirika ya ACRA, WSSCC, SAWA, UNICEF, WaterAid, GIZ, SNV, Plan International, Flaviana Matata Foundation, Msichana Initiative, JALI INTERNATIONAL, FLAVIANA MATATA FOUNDATION, MSICHANA INITIATIVE, JALI Project, TAYOA,  VIGOR na TMARC Tanzania.

No comments: