Thursday, May 19, 2016

HABARI FUPI FUPI KUTOKA BUNGENI MKOANI DODOMA LEO

VIWANDA VIPYA KUJENGWA ILI KUKABILIANA UPUNGUFU WA SUKARI.


Na Tiganya Vincent, Dodoma.                     
                     

Serikali inaendelea na mazungumzo na wawekezaji  wanaokusudia kuwekeza katika viwanda vya  sukari ili kuongeza uwezo wa uzalishaji kwa ajili ya kukabiliana na upungufu wa bidhaa hiyo nchini.


Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati akijibu maswali ya papo kwa papo ya kila Alhamis.


Alisema kuwa lengo la mazungumzo ya kutaka viwanda viweze kuongeza uzalishaji wa sukari ili uweze kufikia tani 420,000 katika kipindi miaka minne ijayo na hivyo kupunguza uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi.


Mhe. Majaliwa alisema kuwa maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vipya ya Sukari ni pamoja na Kigoma, Morogoro na Bonde la Rubada lilipo katika mto Rufiji.


Kuhusu kutojengwa kiwanda cha Sukari katika eneo la Bagamoyo , Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali ilikataa kuruhusu ujenzi wa kiwanda cha Sukari katika eneo hilo baada ya Kamati ya Bunge kushauri kuwa kisijengwe kwa sababu kingehatarisha uhai wa wanyama waliomo katika Mbuga ya Saadan kwa kuwa kingetumia maji mengi kutoka Mto Wami.


Mhe. Majaliwa alisema kuwa   hali hiyo ingesababisha upungufu wa maji ambayo ni tegemeo kwa wanyama wa Mbuga ya Saadan yambao ni muhimu kwa sekta ya utalii nchini.


UPUNGUFU WA SUKARI.

Kwa upande wa upungufu wa sukari nchini , Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali imeagiza  tani  70,000 kutoka nje ya nchi.Alisema kuwa mahitaji ya sukari ni tani 420,000 lakini zilizopo ni tani 320,000 na kuwepo kwa upungufu wa tani 100,000.


Mhe. Majaliwa alisema kuwa Bodi ya Sukari nchini ili kukabiliana upungufu huo imeweka utaratibu wa uagizaji huo ili kuhakikisha Waagizaji wa Sukari nje wasije wakaingiza sukari nyingi kinyume cha inayohitajika na hivyo kuathiri viwanda vya hapa nchini.


Aliongeza kuwa Bodi  hiyo kwa kushirikiana Mamlaka ya Mapato nchini (TRA ) itasimamia kuhakikisha kuwa sukari inayoingiza nchini ndio inayohitajika.Kuhusu bei elekezi ya sukari , Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali inaweka kiwango ili kumlinda mwananchi wa kawaida.


Alisema kuwa bei hiyo zinazingatia gharama zote ikiwemo usafirishaji kutoka zinapoagizwa na kumfikia mlaji.


WAZIRI MKUU APIGA MARUFUKU LUMBESA

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amesema kuwa ni kosa kwa wanunuzi wa mazao ya wakulima kununua mazao kwa vipimo visivyo halali ambavyo havikuidhinishwa na Wakala wa Vipimo nchini.


Amewaagiza viongoizi wote wa Halmashauri,Wilaya na Mikoa yote  nchini kuhakikisha wakulima hawanyonywi kupitia wananunuzi mazao kuliko vipimo halisi kama vile Lumbesa.Mhe. Majaliwa amewaagiza Kamati za Ulinzi na Usalama katika za mikoa na wilaya kusimamia zoezi hili ili mkulima alipe kwa vipimo halali ambavyo ni kilo au gunia liloshonwa kiwanda na sio lile liloongezewa kichuguu(lumbesa).


ELIMU YAONGEZA IDADI YA WATOTO WANAOINGIA LA KWANZA

Kuhusu suala la elimu bure, Waziri Mkuu amesema kuwa lengo ilikuwa na lengo la kumpunzia mzazi mzigo wa ada ya shule za Msingi na Sekondari.Mhe. Majaliwa alisema kuwa ada hizo zilikuwa ni kati ya shilingi elfu 20 na elfu 70.


Amesema kuwa sehemu imebebwa na Serikali ni pamoja na maji,ulinzi,umeme na gharama za mitani mbalimbali.Aidha, Mhe. Majaliwa alisema kuwa baada ya mpango huo wa elimu bure kumekuwepo na ongezeko kubwa na watoto waliondikishwa kujiunga darasa la kwanza mwaka huo  na hivyo kusababisha changamoto ya upungufu wa madawati na madarasa.


Alisema kuwa Serikali inaendelea kuzifanyia changamoto hizo na kutoa wito wadau mbalimbali kuungano mkono juhudi hizo za Serikali.

No comments: