Wednesday, May 4, 2016

BENKI YA KILIMO YATOA MKOPO WA 890MILIONI KWA WAKULIMA WA WILAYA YA KILOMBERO

Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Robert Paschal (aliyesimama) akiwasilimia wakulima wadogo zaidi ya 340 (hawapo pichani) wa mkoa wa Morogoro wakati warsha ya wakulima wadogo zaidi ya 340 wa Mkoa wa morogoro iliyofanyika katika Ukumbi wa Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Lephy Gembe.
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Lephy Gembe (aliyesimama) akiwasilimia wakulima wadogo zaidi ya 340 (hawapo pichani) wa mkoa wa Morogoro wakati warsha ya wakulima wadogo zaidi ya 340 wa Mkoa wa morogoro iliyofanyika katika Ukumbi wa Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero. Kushoto Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Robert Paschal. 
Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Robert Paschal (Kulia) akiwasilisha Mada ya Utambulisho wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo kuhusu Huduma zitolewazo na Benki, Mpango shirikishi wa Kumsaidia Mkulima Mdogo kupata mkopo na utalaam wa kilimo cha kisasa kwa kuwashirikisha wadau wakuu wa Kilimo katika kumkwamua mkulima mdogo wakati warsha ya wakulima wadogo zaidi ya 340 wa Mkoa wa morogoro iliyofanyika katika Ukumbi wa Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Lephy Gembe (Wapili kushoto) akizungumza na Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Robert Paschal (Wapili kulia) wakati warsha ya wakulima wadogo zaidi ya 340 wa Mkoa wa morogoro iliyofanyika katika Ukumbi wa Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Lephy Gembe akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakulima wadogo waliohudhuria warsha ya wakulima wadogo zaidi ya 340 wa Mkoa wa morogoro iliyofanyika katika Ukumbi wa Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.


Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) yatoa mkopo wa 890 Milioni kwa wakulima wa zao la mpunga wanaojishughulisha kilimo cha umwagiliaji katika Kijiji cha Mkula wilayani Kilombero ili kuongeza tija na uzalishaji wa zao la mpunga.

Hayo yaliwekwa bayana na Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Robert Paschal wakati wa warsha ya wakulima wadogo zaidi ya 340 wa Mkoa wa morogoro iliyofanyika katika Ukumbi wa Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.

Bw. Paschal alisema lengo la mkopo huo unaowanufaisha zaidi ya wakulima 350 ni kuongeza tija na uzalishaji wa mpunga ili Kusaidia upatikanaji wa utoshelezi na usalama wa chakula ambao ni endelevu nchini Tanzania na kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.

“Mkopo huu na mengine tunayotoa imelenga kuongeza tija na uzalishaji katika kilimo ili kusaidia kukabiliana na mapungufu hayo na kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo ili kuleta mapinduzi katika kilimo nchini,” alisema Bw. Paschal.

Kwa mujibu wa Bw. Paschal mkopo huo utasaidia shughuli mbalimbali za utayarishaji wa mashamba, kupima ubora wa udongo na virutubisho vinavyohitajika kwenye uzalishaji wa mpunga pamoja na kuwezesha upatikanaji wa pembejeo za kilimo zikiwemo mbegu bora, mbolea na madawa.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa Benki imetoa mkopo kwa ajili ya uwekezaji kwenye ujenzi viwanda vya kusindika mazao, ununuzi wa mitambo na ufungaji wa mitambo ya usindikaji wa mpunga ili kuongeza thamani wa zao hilo.

“Tunaamini mkopo huu utachagiza kuongezeka kwa upatikanaji wa chakula na Pato la Taifa kutokana kuongezeka kwa tija na uzalishaji hivyo kuwa chachu ya ongezeko la thamani, ukuaji wa viwanda vya mazao ya kilimo hivyo kuchangia kuongezeka kwa ajira nchini,” aliongeza. 

Akizungumzia mikakati ya TADB kwa sasa, Bw. Paschal alisema Benki imejipanga kutoa mikopo ya Muda Mfupi, Mikopo ya Muda wa Kati na Mikopo ya Muda Mrefu kwa kutumia njia mbalimbali. Mbinu hizo zinajumuisha pamoja na mambo mengine; mikopo ya moja kwa moja kwa vikundi vya wakulima wadogo wadogo; kutoa mikopo kwa njia ya marejesho taasisi zinazokopesha; utoaji wa mikopo kwa pamoja na kushirikiana na taasisi/benki zingine; pamoja na mikopo ya miundombinu inayolenga kupunguza mapengo ya upatikanaji wa fedha katika minyororo ya ongezeko la thamani ya kipaumbele.

“Kwa kuanzia, TADB imelenga uwekezaji katika maeneo nane (8) ya minyororo ya uongezaji wa thamani ambayo ni: nafaka, kilimo cha mboga mboga, kilimo cha bidhaa za viwanda, mbegu za mafuta, ufugaji wa ng’ombe, ufugaji kuku, ufugaji wa samaki na bidhaa za misitu. Benki pia inajitahidi kusimamia fedha kutoka kwa wafadhili wengine ambazo zimeelekzwa kwenye kuendeleza kilimo,” alisema.

Warsha hiyo ilifunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Lephy Gembe ambaye alitoa rai kwa Wakulima wote waliopata fursa ya kuhudhuria warsha hiyo kujipanga katika kuchangamkia fursa za mikopo inayotolewa na TADB. Mhe. Gembe zingatia mada zilizowasilishwa ili waweze kunufaika na Benki hii na shughuli zinazotolewa na Taasisi zingine za serikali

“Nawasihi mrudishe mikopo mtakayopewa kwa wakati ili wakulima wengine waweze kunufaika zaidi na Benki hii na vile vile kuwezesha Benki kutoa huduma kwenye maeneo mengine ya Tanzania,” alisema.

No comments: