Monday, April 18, 2016

Wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Zantel wapanda miti kwenye hifadhi ya Masingini kama moja ya jitihada za kutunza mazingira.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin akipanda mti katika hifadhi ya Masingini kwa kushirikiana na Bi Nassim Said Mohameid (Kulia) na kushoto ni Mkurugenzi wa Misitu na Maliasili zisizorejesheka wa Zanzibar bwana Sheha Idrissa Hamdani.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin akipanda mti katika hifadhi ya Masingini 
 Mkuu wa Zantel kwa upande wa Zanzibar, Mohameid Mussa (katikakati) akipanda mti kwa kushirikiana na Hamza Zuheri, Meneja wa Mtandao na Vifaa vya mawasiliano wa Zantel (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Misitu na Maliasili zisizorejesheka wa Zanzibar bwana Sheha Idrissa Hamdani (kushoto).
 Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel, Bi Progress Chissenga akipanda miti katika hifadhi ya Masingini. Anayemsaidia kushoto ni Mkurugenzi wa Misitu na Maliasili zisizorejesheka wa Zanzibar bwana Sheha Idrissa Hamdani.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin akipewa maelezo kuhusu hifadhi ya Masingini Bi Nassim Said Mohameid (Kushoto) wakati wa zoezi la upandaji miti lilofanywa na wafanyakazi wa Zantel.
 Wafanyakazi wa Zantel kutoka kushoto Deus Mtena, Winnes Lyaro na Leonard Kameta wakipanda mti katika hifadhi ya Masingini.
 Mwanasheria wa Zantel Bi Julia Kilala akipanda miti kwa kushirikina na watoto wake Noah and Nathan Kilala.
Wafanyakazi wa Zantel na wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo na Maliasili wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza zoezi la upandaji miti.


 Wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Zantel leo wameshiriki katika zoezi la kupanda miti kwenye hifadhi ya Masingini iliyopo magharibi mwa kisiwa cha  Unguja kama  moja ya jitihada zake katika kutekeleza mpango wa kutunza na kuhifadhi mazingira visiwani Zanzibar.

Eneo la hifadhi ya msingini lipo mita 120 kutoka usawa wa bahari na ni eneo lenye vyanzo vingi vya maji  ambavyo vinakadiriwa kutoa lita 27,400,000 kwa ajili ya matumizi ya kila siku ya wakazi wa Zanzibar.

Akizungumza wakati wa upandaji miti, Afsa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya simu ya Zantel,bwana Benoit Janin alisema kupanda miti kutasaidia kuzuia mmomonyoko wa ardhi, kuongeza  rutuba ya udongo na pia kulinda vyanzo vya maji .

‘Kama Kampuni ya simu inayotoa huduma ya mawasiliano kwa wakazi wa visiwani ni lazima tuhakikishe tunatunza na kuhifadhi mazingira kama moja ya  rasilimali muhimu kwa  ajili ya ustawi wa jamii yetu’alisema Bw Janin.

Zoezi hili la kupanda miti limefanyika leo, ikiwa ni wiki moja tu toka uzinduzi wa mtandao wa 4G visiwani hapa, hatua inayoonyesha kuwa kampuni ya Zantel imejipanga katika mpango wa kuhakikisha inalinda na kuhifadhi mazingira kwa kushirikiana na serekali yetu .

Akizungumza baada ya tukio hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar, bwana Sheha Mjaja Juma aliwapongeza wafanyakazi wa kampuni ya simu ya  Zantel kwa kuweza kushiriki kwenye  zoezi hilo  la kutunza na kuhifadhi mazingira.

‘Madhumuni ya zoezi hili la upandaji miti hapa Masingini yamelenga kusaidia jitihada za kutunza na kulinda vyanzo vya maji, msitu pia kuzuia mmonyoko wa ardhi ili kulinda viumbe hai vilivyopo kwenye eneo hilo’ alisema bwana Sheha.

No comments: