Tuesday, April 12, 2016

Wadau wakutana kujadili mabadiliko ya mfumo wa haki jinai nchini


Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Bahame Tom Nyanduga (watatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya wadau wa masuala ya haki jinai (criminal justice) kutoka idara mbalimbali za Serikali na Asasi Zisizo za Kiserikali, muda mfupi baada ya kufungua warsha hiyo, iliyofanyika Makao makuu ya ofisi za Tume, jijini Dar es Salaam mapema leo (Aprili 11, 2016).

Warsha hiyo ya siku moja iliandaliwa na THBUB kwa ushirikiano na Chama cha Wanasheria Tanzania Bara (TLS) na Asasi ya Commonwealth Human Rights Initiative (CHRI) ya nchini India. Ililenga pamoja na mambo mengine kuwahamasisha wadau kujiunga na kushiriki katika jukwaa la Haki na Usalama (justice and security forum) linalotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni. Lengo kubwa la jukwaa hilo ni kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha mfumo wa haki jinai nchini.
 Mkurugenzi wa Asasi ya Commonwealth Human Rights Initiative (CHRI) ya nchini India, Bibi Maja Daruwala akiongea wakati wa warsha ya wadau wa haki jinai, Makao Makuu ya Ofisi za THBUB, jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada katika warsha hiyo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada katika warsha hiyo.
 Picha ya pamoja
 Mhe. Nyanduga na wageni wake, Bibi Daruwala, Mkurugenzi wa Asasi ya Commonwealth Human Rights Initiative na Bwana Anthony Adam, afisa kutoka Asasi ya Open Society Institute of Eastern Africa wakifurahia jambo muda mfupi baada ya ufunguzi wa warsha ya wadau wa haki jinai iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Germanus Joseph wa THBUB)
 Mwenyekiti wa THBUB, Mhe. Bahame Tom Nyanduga akibadilishana mawazo na wabia wa mradi (project partners). Kulia kwa Mhe. Nyanduga ni Mtendaji Mkuu wa Chama cha Wanasheria Tanzania Bara, Bwana Kaleb Lameck Gamaya na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Asasi ya Commonwealth Human Rights Initiative (CHRI), Bibi Maja Daruwala. Kulia ni Bwana Ula Dzenisevich, afisa kutoka CHRI.
Mratibu wa Mradi, Bwana Stephen Msechu akitoa maelezo kuhusu jukwaa la Haki na Usalama wakati wa warsha ya wadau wa haki jinai iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa THBUB, Mhe. Bahame Tom Nyanduga akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa warsha ya haki jinai mapema leo jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wajumbe akichangia hoja wakati wa warsha hiyo.
 

No comments: