Tuesday, April 26, 2016

UVCCM ARUMERU WALAANI KITENDO CHA MWENYEKITI WA MKOA KUMSIMAMISHA KAMANDA WAO

Akizungumza na waandishi mara baada ya baraza hilo kukutana
jana,Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Arumeru, Boniface Mungaya 
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo

Na Woinde Shizza,Arusha

BARAZA la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya
Arumeru umelaani kitendo cha UVCCM mkoani hapa kumsimamisha kamanda wa umoja wa Vijana wa UVCCM wilaya ya Arumeru Mathias Manga kutokana na kuisaliti CCM katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana.

Aidda baraza hilo limelaani tamko lililotolewa wiki iliyopita na
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, Lengai Sabaya na kumtaka ajitathmini na kujipima kama anafaa kuendelea kuwa mwenyekiti wa mkoa,kama ataona hawezi ajing'oe mwenyewe.

Akizungumza na waandishi mara baada ya baraza hilo kukutana
jana,Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Arumeru, Boniface Mungaya,alisema kuwa wanamtambua Manga ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa (NEC),kama Kamanda wao wa vijana.

"Tunalaani tamko lililotolewa na Mkoa na hatumtambui kamanda
mwingine,Kamanda wetu hajatendewa haki,wajumbe wa baraza tumetathmini tamko la Lengai tunaona ni ukiukwaji mkubwa wa kanuni,amepoka madaraka yasiyo yake,kitendo ambacho ni kurudisha chama nyuma badala ya kukijenga.

Mungaya alisema kuwa "Sabaya ajitathmini,ajipime kama anafaa kuendelea kuwa mwenyekiti wa mkoa kwani tunaona akiendelea hivi kukiuka kanuni atakiua chama,ni bora ajing'oe mwenyewe kama anaona hawezi,tunampa siku saba akanushe madai aliyoyatoa dhidi ya kamanda wetu".

Alisema kuwa tamko hilo ni batili na hawalitambui na kumtaka Manga
asivunjike moyo aendelee na haratkati za kukijenga chama hivyo asirudishwe nyuma na changamoto anazokabiliana nazo.Akizungumzia yeye kuwepo kwenye baraza hilo alidai kuwa siku ya kikao alikuwepo ila alikataa kupiga kura ya kumkataa Kamanda wake na kuamua
kutoka nje.

Naye Anjelina Lukumay ambaye ni mjumbe wa baraza hilo kutoka Kata ya
Oldonyosambu,alimuomba Mwenyekiti wa CCM mkoani hapa,Lekule Laizer
kuliangalia suala hilo na kulitafutia ufumbuzi kwani Sabaya amekiuka kanuni za chama.

"Mwenyekiti wa wilaya ametumia kanuni ipi kumkataa kamanda wetu bila
kutushirikisha?hatutakubali kuvurugwa wilaya ya Arumeru,tumepokea kwa
mfadhaiko kauli hiyo kwani Sabaya kachaguliwa hata miezi miwili hana ila
inakuwaje anataka kumtoa Manga tena bila kutushirikisha?alihoji Anjelina
Wiki iliyopita uamuzi wa kumsimamisha Manga ulifikiwa katika kikao cha
baraza la UVCCM mkoa wa Arusha kilichozinduliwa na kaimu katibu mkuu Shaka Hamdu Shaka,ambapo kikao hicho kilikuwa na wajumbe 34 huku 33 kati yao wakipiga kura za ndiyo.

Pia kikao hicho kilitoa onyo kali kwa kamanda wa UVCCM wilaya ya Arusha
Mjini,Longido na Monduli na kuwataka wajipime na kujitathimini kama
wanatosha kuwa makamanda wa UVCCM na wakiona hawatoshi tunaomba wakae pembeni kabla baraza halijawachukulia hatua.Uamuzi wa kumsimamisha Manga ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa (NEC)wilaya ya Arumeru ulifikiwa katika Manga

Akisoma tamko lilitolewa na Kikao hicho cha baraza kikao hicho cha
baraza Katibu wa Hamasa wa (UVCCM) Mkoa wa Arusha, Lucas Nsomi alisema Manga kuanzia wakati huo si kamanda wa Vijana Wilaya ya Arumeru tena kwani amepoteza sifa baada ya kudhibitika kukisaliti chama kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015,kwani wakati wa uchaguzi huo alionekana akifanya vikao vyakufanikisha ushindi kwa UKAWA.

“Kikubwa alichofanikiwa Manga ni kuwagawa vijana wa Arumeru hali
inayopelekea kushindwa kuijenga jumuiya hiyo na kuanzia sasa sio kamanda wa vijana tena wa wialaya hiyo na sipo tayari kufanya naye kazi yoyote ile ndani ya CCM”.

Sabaya alidai kuwa vijana waliompitisha kuwa kamanda lilikuwa ni genge
la wahuni ambao walikuwa wakiendesha vikao vya vijana wenye njaa na kuwa hayupo tayari kuwa Mwenyekiti wa magenge ya vijana wenye njaa na wasaliti ndani ya CCM.

No comments: