Friday, April 29, 2016

UONGOZI WA WANAFUNZI WA CHUO CHA UONGOZI WA FEDHA ZANZIBAR (ZIFASO) WACHAGUA VIONGOZI WAPYA.

Wasimamizi wa uchaguzi wakiwa pamoja na mawakala wa wagombea wakihesabu kura mara baada ya kukamilika zoezi la upigaji kura.
Mawakala na wasimamizi wa uchaguzi wakijumuisha kura ili kujua mshindi katika uchaguzi huo.
Rais mpya wa ZIFASO na Makamu wake Juma Shirazi Hassan na Makamu wake Zuwena Jaku Hassan wakitoa shukrani na nasaha zao baada ya kuchaguliwa kuongoza Jumuia hiyo kwa mwaka 2016/2017. 
Wagombea wa nafasi ya Rais wa ZIFASO Juma Shirazi Hassan a Makamu wake Zuwena Jaku Hassan (wa katikati) wakiongozwa kuingia katika kampasi ya Chuo cha Uongozi wa Fedha Zanzibar kiliopo Chwaka Mkoa Kusini Unguja tayari kwa ajili ya kupiga kura.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Fedha Zanzibar Sabrina Yussuf Shaaban akielezea juu ya utaratibu mzima wa kupiga kura ili kupata viongozi wapya wa ZIFASO .
Mlezi wa wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Fedha Zanzibar Maalim Wazir Hamad akitoa nasaha zake kwa wapiga kura ambao ni wanafunzi wote wa chuo hicho.
Mgeni rasmi katika uchaguzi huo ambae ni Afisa kutoka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mohd Ali Abdalla akiwanasihi wasimamizi na wapiga kura kuendesha uchaguzi katika misingi ya haki.
Mgombea pekee wa nafasi ya Rais wa ZIFASO Juma Shirazi Hassan akipiga kura yake katika uchaguzi huo uliofanyika chuoni Chwaka Mkoa Kusini Unguja.
Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo.

No comments: